... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Alama Yako ya Hatari

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mathayo 13:40-42 Basi, kama vile magugu yakusanywavyo na kuchomwa motoni; ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia. Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maasi, na kuwatupa katika tanuru ya moto, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

Listen to the radio broadcast of

Alama Yako ya Hatari


Download audio file

Nina swali leo, Hivi, unaamini  kama“jehanamu ipo”?, Unaamini kwamba kuna mahali ambapo watu watatengwa na Mungu na kuteswa milele na milele motoni?, Ninauliza hivi kwasababu yale mtu anayoamini kuhusu swala hili, yatakuwa na kishawishi kikubwa katika mfumo wa maisha yake hapa duniani.

Takwimu za utafiti huko Merikani zinaonyesha kwamba, asilimia 76% za wakristo wamarekani wanaamini kwamba kuna mbingu, lakini ni asilimia 32% tu kati yao ndio wanaoamini kwamba jehanamu ni mahali pa kuteswa vibaya milele na milele.  Kuna mwandishi wa gazeti ya New York Times, aliandika hivi miaka miwili iliyopita: “Dhana ya kwamba kuna laana ya milele ya kutengwa na Mungu, haiendani na Biblia, tena haina utetezi kifalfasa na kiuadilifu.  Lakini bado wengi wanavutwa kwa dhana hiyo ki-saikolojia.”  Hili ni oni linaloweza kumsababisha mtu atafakari kwanza.  Sijui yule jamaa alikuwa anasoma Biblia gani!?, lakini tusikilize alichokisema Yesu kuhusu mada hiyo: 

Mathayo 13:40-42  Basi, kama vile magugu yakusanywavyo na kuchomwa motoni; ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia.  Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maasi, na kuwatupa katika tanuru ya moto, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno. 

Hmmm…  Charles Spurgeon alisema hivi:  “Msalaba ni alama ya hatari kwa kukuwekea tahadhari.  Yaani msalaba ni kama kinara cha taa kirefu kilichojengwa mwambao wa bahari ili kuonya mabaharia, yaani kukuonya wewe kwamba kuna uharibifu unawangojea wenye dhambi, ukiwemo wewe kama utaendelea kumuasi Bwana.” 

Kama hakuna moto wa jehanamu, basi hakuna mbingu.  Kwahiyo tupate maono leo.  Kufuatana na alichokisema Yesu, jehahamu ipo kweli kweli. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy