... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Wema ni Dalili ya …

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Luka 6:35,36 Bali wapendeni adui zenu, tendeni mema, na kukopesha msitumaini kupata malipo, na thawabu yenu itakuwa nyingi; nanyi mtakuwa wana wa Aliye juu, kwa kuwa yeye ni mwema kwa wasiomshukuru, na waovu. Basi, iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma.

Listen to the radio broadcast of

Wema ni Dalili ya …


Download audio file

Mengi katika yale aliyoyafundisha Yesu yalitokana na hali halisi ya maisha ya kila siku.  Ndio, aliweza kuongea habari ya imani yetu, lakini aliongea zaidi kuhusu kazi zetu na matendo yetu.

Ni kweli inayosumbua; kwasababu ni rahisi kumwamini Yesu bila kubadilisha namna tunavyoishi.  Sawa, bima yangu ya milele imewekwa saini, imegongwa na muhuri na nimekabidhiwa nakala kwasababu nilimwamini Yesu, basi.  

Lakini sasa; muitikio wa kubadilisha mwenendo wetu, unasumbua kweli.  Ndio maana wengi wanakwepa swala la “toba”.  Kwamfano, Yesu alisema … 

Luka 6:35,36  Bali wapendeni adui zenu, tendeni mema, na kukopesha msitumaini kupata malipo, na thawabu yenu itakuwa nyingi; nanyi mtakuwa wana wa Aliye juu, kwa kuwa yeye ni mwema kwa wasiomshukuru, na waovu.  Basi, iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma. 

Je!, Alitaja adui zetu kweli kweli?  Si utani?  Tungependelea kuwa wakali mno kwao kuliko kuwa wema na kuwaonyesha huruma. Juzi nilisoma maneno yafuatayo … sijui ni nani aliyeyaandika, lakini yalinish’tua sana: 

“Tendo la fidhuli, yaani kukosa adabu ni dalili ya mtu mnyonge na si mwema.  Lakini wema huwa unaonyesha kwamba, mtu ana uwezo wa kujidhibiti.  Sio rahisi kuonyesha wema pale unapokumbuka ufidhuli wa mtu,  Wema ni dalili ya mtu ambaye ameshajikagua vya kutosha, mtu anayejitambua, mwenye hekima.  Amua kuwa mtu mwema kuliko kutetea haki yako kila mara na utakuwa sahihi kila mara kwasababu wema ni dalili ya mtu mwenye nguvu.” 

Ni kweli kabisa. Kadiri mtu anavyozidi kuwa  mwema na mwenye huruma, ndivyo anavyozidi kuonekana machoni pa watu wa ulimwengu kwamba anafanana na Yesu yule anayekiri kwamba anamwamini. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.