Alilipa Deni Langu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Petro 2:21-24 Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake. Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake. Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki. Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa.
Viwango vya riba huwa vinapanda na kushuka, kiwango kikiwa juu inakuwa vigumu kwa waliochukua mkopo na wana madeni kuweza kulipa. Na ni huzuni kwasababu kuna wengine mwishowe wanamezwa na madeni na wanapoteza vyote walivyokuwa navyo.
Ninakuombea usifikie hatua mbaya kama hiyo, na ninashukuru kwamba hata mimi sijafirisika hivyo. Nimeshuhudia watu wakinyanganywa nyumba kwakushindwa kurejesha mkopo waliochukua benki, benki wakaishika nyumba na kuiuza, Yaani ni tukio linalovunja moyo kabisa.
Lakini hata hivyo … mimi ninakiri kwamba nina deni kubwa mno ambalo nisingeweza kulilipa daima. Deni ninalozungumza ni dhambi zangu, Yale makosa yote tuliyoyafanya, hakuna jambo lolote tungeweza kufanya kulipa deni zetu, na kwasababu kiwango alichokitaka Mungu ni utakatifu mkamilifu, basi tungemezwa na madeni yetu, ila…
1 Petro 2:21-24 Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake. Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake. Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki. Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa.
Kama vile mtu fulani alivyowahi kusema, Yesu alikuja kulipa deni ambalo hakulichukua yeye kwasababu sisi tulikuwa na deni ambalo tulishindwa kulilipa. Kinachobaki kwetu, wewe na mimi, ni kumwamini na kuacha kuishi katika dhambi.
Alilipa deni langu na lako, alikufa kifo changu na chako.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.