... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Amani inaanzia Nyumbani

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Kutoka 20:12 Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.

Listen to the radio broadcast of

Amani inaanzia Nyumbani


Download audio file

Sehemu nyingi duniani, ulezi wa watoto ni tofauti sana na jinsi ulivyokuwa zamani.  Leo hii tunaweza kusema kwamba utofauti huo, kwa sehemu kubwa, umeleta madhara mengi katika jamii.

Hakuna awezaye kukana kwamba zamani, watoto wengi walidhulumiwa sana – na wazazi, shuleni, kwenye vituo vya mayatima na cha ajabu, hata na taasisi za dini.  Na bado baadhi ya watoto wanadhulumiwa hivyo.

Watoto wengi hawapati nidhamu, wala hawashiriki kazi za nyumbani.  Kwa kuwa wazazi wengi, mume na mke, wote wako kazini, halafu kwa kujaribu kufidia kutokuwepo kwao, wanawapa watoto kila kitu wanachokipenda wakiwazawadia vitu ambavyo havina maana kabisa.  Sasa mtoto akifeli shuleni, badala ya kumkaripia nyumbani, wanamlaumu mwalimu.

Sasa watoto hao, wakianza kuwa watu wazima, kwa kuwa walidekezwa, wanakuwa na ubinafsi na hawana uwezo wa kustahimili mapambano ya maisha.

Bila shaka, umeshasikia Amri Kumi.  Amri nne za kwanza zinahusu uhusiano wetu na Mungu.  Kwa hiyo, tuulize, Je!  Amri inayofuata inahusu nini?

Kutoka 20:12  Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.

Niweke wazi.  Amri hii inatangulia amri ya mauaji, uzinzi, wizi, uongo na tamaa.  Kwa sababu ukishindwa kutekeleza namba tano vizuri, kuna uwezekano kwamba na zingine zote zinazofuata zitakushinda.

Ninyi wazazi, fundisheni watoto wawaheshimu.  Baada ya kuwaongoza kwa Yesu, hili ni jambo lililo muhimu kuliko yote ungewatendea.   

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy