Amani Pande Zote
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Wafalme 4:24,25 Kwani Sulemani alikuwa akitawala nchi yote upande huu wa Mto, toka Tifsa mpaka Gaza, juu ya wafalme wote wa upande huu wa Mto; naye alikuwa na amani pande zake zote. Yuda na Israeli wakakaa salama, kila mtu chini ya mzabibu wake na chini ya mtini wake, tokea Dani mpaka Beer-sheba, siku zote za Sulemani.
Ninajiuliza ni mapambano gani unayokabiliana nayo muda huu? Labda ndoa yenye shida kubwa, labda hali yako ngumu ya uchumi, labda kujiona kwamba hufai, labda hofu ya mambo yanayokuja? Haijalishi ni yapi, kwa vyo vyote yanakuibia amani.
Ni kweli, hua sote tunapitia vipindi mbali mbali katika maisha. Kuna mara mambo yanaenda sawa tu. Pia kuna wakati hayaendi sawa. Na hata kama kwa sura ya nje tunaonekana kuwa sawa, humu ndani katika mawazo yetu na hisia zetu, tukitafakari hiki na kile, kwa kweli amani hamna sawa.
Jana tuliona jinsi Mungu aliyemwahidi mfalme mpiganaji shujaa wa Israeli, Daudi kwamba mwanae atatawala kipindi cha amani ya ajabu. Sasa tunajua kwamba Daudi alipigana vita mara nyingi kiasi cha kutoweza kuhesabu tena mara zile zote yeye na taifa la Israeli walivyoweza kunusurika.
Hata hivi, Mungu aliahidi amani kwa ajili ya mwanae Daudi na watu wake. Je! Ahadi ile ilikuwa hakika? Sikiliza ilivyotokea:
1 Wafalme 4:24,25 Kwani Sulemani alikuwa akitawala nchi yote upande huu wa Mto, toka Tifsa mpaka Gaza, juu ya wafalme wote wa upande huu wa Mto; naye alikuwa na amani pande zake zote. Yuda na Israeli wakakaa salama, kila mtu chini ya mzabibu wake na chini ya mtini wake, tokea Dani mpaka Beer-sheba, siku zote za Sulemani.
Sasa, baada ya miaka hiyo yote, ahadi ya Mungu ihusuyo amani bado inasimama pale pale. Ndiyo maana Yesu anaitwa Mfalme wa Amani. Katika yeye, amani ya Mungu ipo kwa ajili yako.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.