Angali Sana Jinsi Unavyoenenda
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Waefeso 5:15-17 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda, si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu. Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.
Tumepewa kuishi maisha mara moja tu hapa duniani na muda wetu unaenda taratibu siku baada ya siku. Kwa hiyo, niulize. Utatumiaje siku yako ya leo? Kesho, utaitumiaje?
Inabidi tujiulize maswali yale mara kwa mara; tukijitenge kidogo na mambo yanayotusonga na kudai muda wetu kana kwamba yana haki ya kututawala; badala ya kukusudia vipaumbele vyetu katika muda tunaobakiza duniani, ili tuweze kupanga maisha yetu ilete mtikiso na urithi tutakaouachia watu wengine.
Kwa hiyo acha nikuulize tena, Utaenendaje siku ya leo hii? Kesho utaishije? Yashike mawazo hayo kwanza wakati tunamsikiliza Mungu anavyoongea kuhusu mada hii:
Waefeso 5:15-17 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda, si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu. Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.
Sasa katika mistari hii, Mungu anataka kusema nini? Anataka uwe makini sana kuishi kwa hekima. Ina maana, usitapanya maisha yako kwa vitu ambavyo havina maana. Usiwe mjinga. Ni hasara tupu. Bali jaribu kutafuta kila fursa ya kutenda mema siku hizi za uovu.
Je! Ni fursa gani unazo mbele yako leo hii na kesho za kutenda mema; kuonyesha wengine upendo wa Mungu; kuwatia moyo; kuwainua; kuwasaidia … kuwaambia habari za Yesu?
Angalia sana jinsi unavyoishi.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.