Bure Kabisa
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Wafilipi 3:4-7 Walakini mimi ningeweza kuutumainia mwili. Mtu ye yote akijiona kuwa anayo sababu ya kuutumainia mwili, mimi zaidi. Nalitahiriwa siku ya nane, ni mtu wa taifa la Israeli, wa kabila ya Benyamini, Mwebrania wa Waebrania, kwa habari ya kuishika torati, ni Farisayo, kwa habari ya juhudi, mwenye kuliudhi Kanisa, kwa habari ya haki ipatikanayo kwa sheria sikuwa na hatia. Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo.
Sehemu kubwa katika ukuaji, yaani kuwa mtu mzima kwa kupitia miaka ya ujana, ni kujifunza kutokuwategemea wengine na kuanza kujitegemea wewe mwenyewe, Na kwa sehemu ni sahihi, ndivyo inavyotakiwa iwe. Lakini pana mtego.
Watoto wetu walipokuwa watu wazima, ilikuwa furaha sana kwetu kuona namna walivyoanza kuacha kututegemea sisi kama wazazi waon na kuanza kutegemea yale tuliyowafundisha. Hii ni maana ya kujitegemea. Sawa kabisa. Sasa, mtego uko wapi? Ngoja nikuelezee.
Mtu akijitathmini kuhusu yale anayoweza kufanya mwenyewe, ni rahisi kuanza kutegemea vipaji na vipawa vyake kuliko kutegemea neema ya Mungu. Sikiliza alivyoeleza Mtume Paulo:
Wafilipi 3:4-7 Walakini mimi ningeweza kuutumainia mwili. Mtu ye yote akijiona kuwa anayo sababu ya kuutumainia mwili, mimi zaidi. Nalitahiriwa siku ya nane, ni mtu wa taifa la Israeli, wa kabila ya Benyamini, Mwebrania wa Waebrania, kwa habari ya kuishika torati, ni Farisayo, kwa habari ya juhudi, mwenye kuliudhi Kanisa, kwa habari ya haki ipatikanayo kwa sheria sikuwa na hatia. Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo.
Paulo, kusema ukweli alikuwa mtu wa ajabu. Alifuata kanuni zote za Mungu na katika kujitegemea kwake, alifikiri kwamba amefaulu kumpendeza Mungu. Hadi siku ile aliyokutana na Yesu. Ndipo alipogundua kwamba ukoo wake pamoja na uwezo wake ulikuwa bure kabisa.
Usiwe mtu wa kujitegemea. Uwe mtu wa kutegemea neema ya MUNGU.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.