Bwana Atakulinda
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Zaburi 3:3-5 Na Wewe, BWANA, U ngao yangu pande zote, utukufu wangu na mwinua kichwa changu. Kwa sauti yangu namwita BWANA naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu. Nalijilaza nikalala usingizi, nikaamka, kwa kuwa BWANA ananitegemeza.
Zamani, dhana ya kwamba mfalme anapaswa kuwa kwanza mtumishi ilikuwa haipo kabisa. Kusikia maneno hayo mawili katika sentensi moja ni wakati mtu anaeleza habari ya mtumishi wa mfalme au watumishi wake tu.
Sasa tupige hatuna ingine. Dhana ya mungu fulani kuwa mtumishi ilikuwa haieleweki kabisa. Miungu mataifa mengine walioitumikia walikuwa sanamu za uongo ambazo watu walijaribu kutuliza ili ghadhabu yao dhalimu isiwaangukie.
Lakini hatuwezi kuacha kueleza kwamba Mungu wa Israeli alikuwa amefanya agano nao, au mapatano kwamba wakimheshimu, atawaheshimu; wasipomheshimu, atawalaani. Lakini hata ndani ya agano lile, dhana ya Mfalme Mtumishi, Mungu Mtumishi ilikuwepo wazi wazi. Mfalme Daudi aliandika hivi:
Zaburi 3:3-5 Na Wewe, BWANA, U ngao yangu pande zote, utukufu wangu na mwinua kichwa changu. Kwa sauti yangu namwita BWANA naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu. Nalijilaza nikalala usingizi, nikaamka, kwa kuwa BWANA ananitegemeza.
Mungu huyu wa Israeli, Mungu mmoja wa kweli, Mungu ambaye angetuma, hatimaye, Mwanae Yesu kufa kwa ajili ya dhambi zao na za kwetu pia … tangu mwanzo kabisa alikuwa Mfalme Mtumishi. Yule ambaye angelinda watu wake, na kuwapa heshima na tumaini, Mungu ambaye angewajibu wakati wanamwomba na kuwapa amani.
Nisikilize sasa, hakuna kilichobadilika. Mungu hajabadilika.
Unaweza kupumzika na kulala ukifahamu kwamba utaamka salama kwa sababu Bwana anakufunika na kukulinda.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.