Chanzo cha Imani ni Kusikia
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Warumi 10:17 Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.
Kwanini watoto wanahitaji kutiwa moyo lakini pia kurudiwa na wazazi na walimu, mara kwa mara ili waweze kujitegemea na kuwa na matumaini ya namna watakavyoishi katika mfumo wa jamii?, Lazima wazoezwe mara nyingi sana. Kwanini ni hivi?
Na kwa kweli, swali langu ni zuri kabisa hata kama nimeliuliza mimi mwenyewe. Kwa nini mtu hawezi kuwaambia watoto kitu mara moja tu na kikatekelezwa daima? Kila mzazi atafahamu usumbufu wa kuwaambia watoto jambo lile lile! Jamani! Kwa nini hawasikii?!
Sasa, ebu fikiria anavyojisikia Mungu pale watu kama wewe na mimi, tunapomsumbua … Kwanini hawanisikii?
Kwa kweli, ni swali zuri, Je! Kwa nini hatumsikilizi Bwana? Jibu ni kwamba … ni kwa sababu hatusikii.
Warumi 10:17 Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.
Jibu lililopo kwa watu wa Mungu wengi lina sehemu mbili. Kwanza, hawafungui Biblia zao, pili wakizifungua (au wakisikiliza ujumbe kama huu wetu), hawapokei Neno la Mungu mioyoni mwao.
Jana tuliongelea habari za hatari ya kukubali kushawishika na wasioamini, na athari zake kwa imani zetu. Leo tunapata jambo zuri ambalo ni kinyume cha vishawishi vile. Yaani ni uwezo unaotokana kwa kumsikiliza Mungu na kupokea Neno lake mioyoni mwetu, uwezo unaoimarisha na kukuza imani yetu.
Wewe vipi? Ni kipi kinachokushawishi zaidi? Rafiki zako wasioamini, mambo ya siasi yasiyoeleweka kutoka kwenye mtandao, filamu chafu unazoangalia ndani ya simu yako … au ni Neno la Mungu mwenyewe? Ni dhana yenye tafakari kabisa.
Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.