Dhana Inayochukiza Sana
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Warumi 10:9 Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.
Haijalishi unaishi chini ya mfumo gani wa serikali, siku hizi sote tunatamani kuwa huru, kuamua sisi wenyewe tutakavyokuwa bila watu wengine kutwambia yatupasayo kuyafanya.
Shauku la uhuru, naona ni sifa bainishi ya kibinadamu. Kwa hiyo dhana ya mwingine kututawala, kwa ujumla ni dhana inawachukiza karibia watu wote. Hata hivi, Neno la Mungu linasema :
Warumi 10:9 Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.
Kwa kweli si kusema tu “Yesu ni Bwana”, bali ni kuliamini kwenye kiini cha moyo wako na kumpokea kama Bwana wako na kuishi sambamba na kukiri kwako. Inahusu kukubali kidete aongoze maisha yako daima; awe na mamlaka juu yako.
Haishangazi kusikia kwamba wasiomwamini Yesu wanachukizwa na madai yake, lakini kinachohuzunisha zaidi ni kwamba hata Wakristo baadhi wanachukizwa pia. Lakini ni kweli kinzani kwamba wakati mtu anampokea Yesu kabisa kama Bwana juu ya maisha yake, hapo tu ndipo anawekwa huru kweli kweli. Hapo tu ndipo anaokolewa na dhambi iliyokuwa inamsumbua katika sekta zote za maisha yake, dhambi iliyomnyang’anya ule uhuru tuliyokuwa tunautamani sisi sote kila wakati.
Je! Ninaweza kukuuliza kama umefikia wapi katika swala hili la kukubali Utawala wa Kristo juu ya maisha yako? Kwa sababu wengi wanaamini lakini ni wachache wanajiweka chini yake. Wengi wanakiri kwamba wao ni Wakristo lakini wanakataa kukubali kwamba Neno la Mungu ni kweli na kulitii.
Ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.