Furahia Mambo Bila Kunung’unika
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Wafilipi 2:14,15 Yatendeni mambo yote pasipo manung’uniko wala mashindano, mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu.
Kwa asilimia kubwa, mambo ya muhimu katika maisha yako yanaendelea shwari mahusiano na watu wengine, afya yako, uchumi lakini kuna kile kitu kimoja ambacho bado kinakusumbua sana.
Tunataka kulalamika na kunung’unikia kile kitu kimoja kana kwamba hatuoni mambo mengine yote ambayo yanaendelea vizuri maishani mwetu. Kwa nini tunafanya hivyo? Nafikiri tabia ya mwanadamu ndivyo ilivyo.
Kwa hiyo, tunaweza kushtuka tukimwangalia Yesu na kugundua kwamba hakuwahi kunung’unika hata siku moja. Je! Umeshawahi kusoma maneno ya manung’uniko yaliyo toa mdomoni mwake hata mara moja? Hamna.
Hata wakati ule aliosalitiwa na Yuda na kuhukumiwa, akapigwa na kudhihakiwa na hatimaye kugongelewa na misumari kwenye msalaba. Hakutamka hata neno moja la manung’uniko!
Wafilipi 2:14,15 Yatendeni mambo yote pasipo manung’uniko wala mashindano, mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu.
Kwa mistari hiyo, Mungu anatuambia tufanye mambo mangapi pasipo manung’uniko wala mashindano? Mambo yote! Kwa nini sasa tutende yote bila manung’uniko? Tupate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila.
leo hii, tupate maono kwa pamoja. Haijalishi mambo yangekuwia vigumu kiasi gani, acha kulalamika, acha kunung’unika, acha mashindano ya maneno … Songa mbele tuu…
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.