Gharama Iliyolipwa Ili Uweze Kuanza Upya
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Petro 1:18,19 Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu; bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani ya Kristo.
Tukitafakari kwanza kuhusu jinsi watu wengine walivyojitoa na kugharimiwa ili tuweze kufikia mahali tulipo kwa kweli inashangaza. Ni kwa sababu shukrani ina nguvu nyingi katika maisha ya mwanadamu.
Nikitafakari marafiki waliosimama nami vipindi vigumu sana. Au mke wangu aliyekuwa kando kupitia mabonde na milima ya huduma na maisha yangu. Ninaduaa kabisa nikifikiri jinsi watu walioweza kunitendea mema hayo yote … kwa ajili ya mimi!
Wewe vipi? Ni akina nani maishani mwako waliojitolea kwa ajili yako? Ukitafakari kujitoa kwao, unajisikiaje? Yaani inakunyenyekeza lakini pia, inapendeza mno, si kweli? Lakini kuna mmoja ambaye kujitoa kwake kumebadilisha watu kabisa.
1 Petro 1:18,19 Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu; bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani ya Kristo.
Ukitafakari ilivyomgharimu Yesu ili akuokoe, ukitafakari alivyoteseka , kwa kweli itabadilisha mtazamo wako, hisia zako na jinsi utakavyoendela kuishi maisha yako. Shukrani ina nguvu nyingi katika maisha ya mwanadamu. Uiruhusu ikubadilishe, kwa sababu …
Ulikombolewa na damu ya thamani ya Kristo wakati alikufa kwa ajili yako.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.