Gharama ya Mwisho
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Warumi 12:1 Basi ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai takatifu ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.
Ujumbe wa msingi wa Ukristo unaitwa “Habari Njema”- ni kwamba Yesu, Mwana wa Mungu, alifanyika mwanadamu na alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, ili gharama iliyodaiwa na haki ya Mungu ilipwe. Halafu tukimwamini huyu Yesu, tunapokea karama ya uzima wa milele.
Ni habari njema kabisa. Yaani, ni habari njema mno kuliko zote ambazo binadamu – wewe na mimi tukiwemwo – tungeweza kupata. Na kama hujapokea ujumbe huo, ningekusihi leo hii uupokee na moyo wako wote, ukamwamini Yesu – roho, nafsi, mwili.
Swali lililopo ni hili. Baada ya kumwamini Yesu na kutegemeza maisha yako yote kwake kwamba yeye ni njia pekee iwezayo kukufikisha kwa Baba, kinachofuata ni kipi? Je! Tuendelee kuishi kama kawaida, bila mabadiliko yo yote? La hasha!
Warumi 12:1 Basi ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai takatifu ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.
Mwitikio unaotakiwa dhidi ya yote Mungu aliyotutendea wakati alitoa vyote pale Msalabani ni kufanya kama alivyofanya. Kutoa maisha yetu kama dhabihu iliyo hai kwa ajili yake – dhabihu inayompendeza.
Yesu alitoa gharama ya mwisho kwa ajili yako. Mwitikio sahihi, mwitikio pekee ni kumtolea maisha yako kama dhabihu iliyo hai.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.