God’s Mercy
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Petro 1:3 Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu.
Mimi nina imani kubwa kwamba hatuwezi kamwe kutumia muda mwingi wa kupita kiasi kutafakari na kusimulia habari za kufufuka kwa Yesu Kristo. Ni kwasababu tukio lile la Yesu kufufuka kutoka mautini limebadilisha kila kitu!
Cha huzuni, watu wengi wanatumia muda mchache sana kutafakari ufufuko wa Yesu, halafu wanajiuliza, ni kwanini hali ya maisha yao hayaendani na imani zao ndani ya Yesu; kwanini wanakatishwa tamaa?
Mimi ninaelewa hali ya maisha ya kila siku. Mtu anaamka, anafanya shughuli zake na hata kama anamwamini Yesu na kufa kwake pamoja kufufuka kwake … ni kama hayana uhusiano na mambo anayokumbana nayo mchana kutwa siku baada ya siku.
Kwahiyo, kama wewe husikii maunganisho kati ya imani yako na hali halisi ya maisha yako ya kila siku, basi pokea yafuatayo:
1 Petro 1:3 Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu.
Kiunganishi kati ya ufufuko wa Yesu uliotokea miaka elfu mbili iliyopita na maisha haya ya kisasa yanayoenda kasi ni kwamba, kupitia rehema zake, ametukirimia maisha mapya!
Tafadhali nisikilize. Haitakiwi tuishi maisha ya kale yenye dhambi na ubinafsi, bali maisha mapya ya kujitolea hata kuteswa, lakini pia maisha yenye utukufu, furaha, amani na uwezo. Pia … tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu.
Kristo amefufuka! Na wewe pia umefufuka!
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.