... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Haina Makona

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Waebrania 13:16 Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu.

Listen to the radio broadcast of

Haina Makona


Download audio file

Zamani za kale, watu wa Mungu walitoa sadaka za kuteketezwa kwenye madhabahu. Kwetu siku hizi tunaona kama ni jambo geni kabisa lakini zamani ilikuwa kawaida.  Sasa sisi tumejaliwa kwa sababu hatuhitaji kuzitoa tena … au!

Ni kweli, siku hizi hatutoi dhabihu za wanyama. Watu walizitoa wakati ule kwa sababu ya dhambi, sadaka zilete upatanisho; na kwa sababu zingine pia.  Lakini kama unamwamini Yesu, huna haja tena ya kutafuta upatanisho kwa ajili ya dhambi zako kwa sababu kupitia dhabihu yake moja ya kujitolea pale msalabani, dhambi zako zote zimesamehewa, mara moja na kwa milele. 

Haleluya.  Hakuna sababu ya kutoa dhabihu tena. Lakini ngoja kwanza, kwa sababu suala la kusema “dhambi zangu zimesamehewa” siyo mwisho wa habari, bali ni mwanzo wa hatua za kuishi maisha mapya, maisha yaliyobadilika, maisha yanayolenga kumfuata Yesu, maisha yenye nia ya kushirikisha wengine upendo wake, maisha ya kutikisa ulimwengu na kuleta mabadiliko ya kweli. 

Waebrania 13:16  Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu. 

Hayo hayatakiwi mtu aelewe sayansi ya hali ya juu, si kweli?  Lakini ni rahisi kusahau ukweli huo kwenye pirikapirika za maisha.  Lakini pia ni rahisi kujishughulisha na mambo yetu ya kutafuta starehe na anasa hadi tunasahau kushirikiana na wengine katika mahitaji yao; tukasita kujitolea kabisa kwa ajili ya kuwasaidia wengine.  Kumbe, dhabihu bado zinahitajika tena zinampendeza Mungu sana. 

Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu. 

Unaona, haina makona. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy