Hakuna Nafasi Kwa Ajili ya Mwokozi
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Luka 2:7 Akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng’ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.
Sasa tumeifikia Sikukuu ya Krismasi kwa mara nyingine tena. Sikukuu katika mlolongo wa Krismasi nyingi. Sasa sikukuu hii ya leo, je! Unaichukuliaje? Leo, Utafanyaje?
Habari ya Krismasi inafahamika sana. Mariamu, akiwa mjamzito kwa uweza wa Roho Mtakatifu akiwa pamoja na Yusufu aliyemposa (si baba wa mtoto yule), walikwama wote wawili sehemu inayonuka, sehemu ya baridi pale wanapofungia mifugo usiku. Kwa nini? Ni kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.
Kwa nini walikosa nafasi kwenye gesti? Ni kwa sababu watu wengi walikuwa wametikiswa na amri ya Rumi iliyohusu sensa, amri ya kulazimisha kila mtu kurudi makwao ili ahesabiwe.
Ndiyo maana Mariamu na Yusufu walikuwa pale Bethlehemu. Hii ni sababu walikosa nafasi katika nyumba ya wageni. Mambo ya dunia hii yaliwanyima nafasi – mambo ya dunia yalimnyima nafasi hata Mwokozi wao! Alisukumiwa pembeni kabisa na matukio ya ulimwengu huu; alisukumiwa huko nje kwenye zizi la mifugo.
Luka 2:7 Akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng’ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.
Najiuliza kama hiyo ndiyo habari ya Krismasi. Yesu, Mwokozi wa ulimwengu kusukumiwa mbali na ulimwengu kwa sababu hakuna aliyetaka kumpa nafasi.
Kwa hiyo niulize tena, je! Wewe utaichukuaje siku hii? Ujio wa Mwokozi aliyekuja kukuokoa na dhambi zako, akuletee msamaha, akuletee maisha mapya, uzima wa milele? Au uko bize sana ukijishughulisha na mambo ya dunia hii tu?
Kumbuka sasa: Andaa nafasi kwa ajili ya Yesu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.