... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Ikawa Siku Moja …

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Luka 2:5,6 Ili aandikwe pamoja na Maramu mkewe, ambaye amemposa, naye ana mimba. Ikawa, katika kukaa huko, siku zake za kuzaa zikatimia.

Listen to the radio broadcast of

Ikawa Siku Moja …


Download audio file

Ikawa siku moja, Mariamu na Yusufu walienda Bethlehemu na mtoto mchanga Yesu akazaliwa na kulazwa katika hori ya kulia ng’ombe.  Inasomeka kama hadithi ya watoto.

Unajua ninachofikiri mimi? Naona kama Shetani anataka tuchukue habari ya Krismasi kama hadithi tu … tukiiangalia kwa mbali kama hadithi, hadithi ya watoto. Hii ni kwasababu anajua kwamba tukiichukua hivyo hatutaelewa maana yake. Tusipoelewa maana ya Krismasi, basi tutakosa kufahamu lengo la Yesu kuja hapa duniani na Shetani atakuwa ameshinda tayari. 

Haijalishi unaamini nini, unijibu, hivi, unaonaje habari hii ya Krismasi?  Inakutikisa moyoni au umeshazoea hadi unaichukulia kama kawaida, yaani kama hadithi isiyo kwelivile!

Ukweli wa Krismasi ni habari ya changamoto nyingi na hali ngumu kabisa. 

Luka 2:5,6  Ili aandikwe pamoja na Maramu mkewe, ambaye amemposa, naye ana mimba.  Ikawa, katika kukaa huko, siku zake za kuzaa zikatimia.

Mariamu alikuwa mjamzito tena alikuwa hajaolewa (mimba ilitoka kwa Roho Mtakatifu, ila sidhani kama watu wangeiamini!).  Yusufu naye lazima awe na mawazo mengi hata kama alikuwa amemwamini malaika aliyemwambia hali halisi ya mambo. Walikuwa wameshatembea siku za kutosha kutoka Nazareti kwenda Bethlehemu na sasa mtoto Yesu alizaliwa kwenye pango la kulaza mifugo na kulazwa kwenye hori la kulia ng’ombe.  

Hii si hadithi iliyotungwa bali ni hali halisi ya upendo wa Mungu; upendo wake kwako.  Yeye alimtuma Mwanae kwa ajili yako, ili akuokoe na dhambi zako na kukupa karama bure ya uzima wa milele.  Hii ndiyo maana halisi ya Krismasi. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.