Hata Wakati wa Uzee Wako
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Zaburi 92:12-15 Mwenye haki atasitawi kama mtende, atakua kama mwerezi wa Lebanoni. Waliopandwa katika nyumba ya BWANA watasitawi katika nyua za Mungu wetu. Watazaa matunda hadi wakati wa uzee, watajaa utomvu, watakuwa na ubichi. Watangaze ya kuwa BWANA ni mwenye adili, mwamba wangu, ndani yake hamna udhalimu.
Kuna jambo linaloleta huzuni nyingi siku hizi hata kuwa kama tauni ulimwenguni, ni kuona wazee, wanaume kwa wanawake – watu wano uzoefu mkubwa na busara kutokana na umri wao – jinsi wanavyojiuzuru katika maisha.
Kwa kusema wanajiuzuru katika maisha ninataka kusema hivi, wanaacha kuhudumia watu wengine. Wanaacha kutoa vipawa vyao, vipaji na muda (na muda mwingi wanao sasa) wasiwabariki watu wengine tena. Ndiyo, najua kwamba ni kawaida mtu kutoka kwenye ajira na kustaafu akifika umri uliopangwa huko kwao. Hii haina shida.
Lakini wazee wengi sana wanaamua kwamba tokea sasa … Yote yananihusu mimi. Nitazunguka dunia kwa kutalii. Nitatumia muda wangu nikifanya vitu vinavyonipendeza mimi. Kwa hiyo, kidogo kidogo, wanazidi kulenga wao wenyewe na kutapanya bure vipaji vyao, uzoefu wao na hekima yao.
Haitakiwi iwe hivyo kwa sababu kadiri mtu anakuwa na ubinafsi kwa kulenga mambo yake tu, ndipo maisha itazidi kukosa kumridhia. Kwa hiyo, yafuatayo ni mpango wa Mungu kama una hamu kuujua:
Zaburi 92:12-15 Mwenye haki atasitawi kama mtende, atakua kama mwerezi wa Lebanoni. Waliopandwa katika nyumba ya BWANA watasitawi katika nyua za Mungu wetu. Watazaa matunda hadi wakati wa uzee, watajaa utomvu, watakuwa na ubichi. Watangaze ya kuwa BWANA ni mwenye adili, mwamba wangu, ndani yake hamna udhalimu.
Ni kweli, kadiri mtu anavyozeheka, mwili wake utaendelea kumtazamisha kwamba anakaribia kufa na kuondoka. Lakini wao ambao ni mali ya Bwana, walikusudiwa kuendelea kuzaa matunda katika uzee wao … kama vile miti chipukizi yenye kustawi. Kazi ya wazee ni kuonyesha watu wote kwa mienendo yao kwamba Bwana yu mwema.
Mzee, usijiudhuru katika maisha haya. Endelea kuzaa matunda.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.