... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Hatima ya Ajabu Mno

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mwanzo 41:41,42,44 Farao akamwambia Yusufu, Tazama, nimekuweka juu ya nchi yote ya Misri. Farao akavua pete yake ya muhuri mkononi mwake, akaitia mkononi mwa Yusufu; akamvika mavazi ya kitani nzuri, na kumtia mkufu wa dhahabu shingoni mwake ... Farao akamwambia Yusufu, Mimi ni Farao, na bila amri yako, mtu asiinue mkono wala mguu katika nchi yote ya Misri.

Listen to the radio broadcast of

Hatima ya Ajabu Mno


Download audio file

Je!  Umewahi kufikiri kwamba inawezekana Mungu anakuandalia mambo makuu kwa kutumia taabu ambazo unazopitia?  Yamkini ni vigumu kukubali dhana hiyo wakati bado unateswa, lakini mara nyingi Mungu anafanya hivyo.

Yusufu ni shujaa mojawapo ndani ya Agano la Kale.  Ndugu zake walimwonea wivu na kumfitinisha wakitaka kumwangamiza.  Lakini mwisho wa siku, walimwuzia watu waliompeleka utumwani.

Baada ya kupelekwa katika minyororo hadi Misri, alizalilishwa kwa kusingiziwa ubakaji na alikaa gerezani miaka mingi.  Lakini kila wakati alinyimwa haki na kutendewa jeuri, Yusufu aliendelea kutenda mema tu; aliendelea kujitahidi kutumia vipaji na vipawa vyake.

Mwanzo 41:41,42,44  Farao akamwambia Yusufu, Tazama, nimekuweka juu ya nchi yote ya Misri.  Farao akavua pete yake ya muhuri mkononi mwake, akaitia mkononi mwa Yusufu; akamvika mavazi ya kitani nzuri, na kumtia mkufu wa dhahabu shingoni mwake … Farao akamwambia Yusufu, Mimi ni Farao, na bila amri yako, mtu asiinue mkono wala mguu katika nchi yote ya Misri.

C.S. Lewis alidokeza kwamba taabu mara nyingi zinaandaa watu wa kawaida kutenda makuu.  Ndio, labda wewe hautakuwa Waziri Mkuu wa Misri, lakini acha nikwambie kwamba yaliyo bora bado yanakungoja.

Licha ya yote ambayo unakabiliana nayo maishani, endelea tu kutenda mema kwa sababu inawezekana Mungu, kwa kupitia hayo anakuandaa kwa mambo makuu.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.