Hekima ya Kale (2)
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Tito 2:3,4 Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao mema; ili wawatie wanawake vijana akili, wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao.
Mwanasaikolojia yoyote atakwambia kwamba, licha ya jitihada zinazofanyika katika sehemu fulani ya jamii kutokana na utofauti wa kijinsia, kuna utofauti wa msingi tena mkubwa mno kati ya wanamume na wanawake.
Jana tulianza mada fupi ya mfumo wa kale kuhusu nafasi tofauti ya wanaume na wanawake katika jamii na ndani ya familia, kulingana na Neno la Mungu.
Tulianza na wazee wanaume kuwa vielelezo vya kuigwa katika jamii, wawe wenye kiasi, wastahivu, wenye busara, wazima katika imani na katika upendo na katika saburi. Nadhani hakuna awezaye kupinga haya. Sasa, vipi kwa wazee wa kike? Wanapaswa kuwa na mwenendo gani?
Tito 2:3,4 Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao mema; ili wawatie wanawake vijana akili, wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao.
Kuna utofauti mkubwa kati ya wanaume na wanawake, ni kwamba akina mama mara nyingi wanaelekea kupiga domo na kusema wengine, hususani wamama wazee, kwa kuwa hawana kazi nyingi sana.
Ninyi akina mama wazee, umbea sio wito wako. Pia usilewe kwa kutumia pombe kama vile wengine wengi wanavyofanya, wakitembea huku na huko jioni, kwa kupoteza muda tu. kama wewe ni mama mzee kazi yako ni hii: Ni kufundisha wanawake vijana namna ya kupenda waume zao na namna ya kulea watoto wao vizuri.
Labda hayo hayawezi kuonekana sahihi kwenye siasa ya kisasa, lakini mtu akiyatafakari hayo, itamwia vigumu kuleta ubishi. Ukizingatia pia changamoto ambazo wanawake vijana wanazipitia katika karne hii ya 21, kweli wanahitaji zaidi, ushauri na mafundisho.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.