Huko Ng’ambo
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Yohana 14:1-3 Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.
Je! Umewahi kuhangaika ukitafakari kinachokusu huko baada ya kifo?… wakati utakapo vuta pumzi yako ya mwisho? Najua kwamba si wewe tu, unafadhaishwa na mawazo kama hayo.
Niruhusu nitoe mfano huu nilipata kuusikia hivi karibuni.
Mgonjwa fulani alimgeukia daktari wake wakati akitaka kutoka kwenye chumba cha vipimo akisema, “Daktari, mimi ninaogopa kufa. niambie, kuna nini huko ng’ambo?”
Daktari alijibu kwa sauti ndogo, akisema, “Sijui …”
Hujui! Wewe ni Mkristo na hujui kinachosubiri mtu baada ya kifo?” Daktari alipokuwa akitoka ndani ya chumba; upande wa pili alisikia kukwaruza na kulia, kumbe mbwa alijitupa ndani ya chumba akimrukia daktari kwa furaha kubwa. Ndipo mganga akamgeukia mgonjwa yule akisema, “Je! umeona? Mbwa wangu hajawahi kuingia ndani ya chumba hiki hata mara moja, hakujua kinachomgojea humu, alichokijua tu ni kwamba bwana wake alikuwemo na wakati mlango ulifunguliwa, alijitupa mara moja ndani bila hofu. Mimi sijui mengi kuhusu mambo yanayoningojea baada ya kufa, ili nafahamu kitu kimoja … Bwana wangu ndipo alipo na kujua hilo inatosha.”
Yohana 14:1-3 Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.