Imani Iliyo Hai
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Yakobo 1:21,22 Kwa hiyo wekeeni mbali uchafu wote na ubaya uzidio, na kupokea kwa upole neno lile lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu. Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu.
Mwanariadha mwenye uwezo ni mtu wa ajabu. Haijalishi anacheza pamoja na wengine katika timu au anashindana na mtu mmoja mmoja, lazima afanye mazoezi magumu mno ili aweze kuwa bora vyakutosha.
Kwahiyo, kama ukishangilia timu yako unayoipenda zaidi au mwanariadha, sasa ukiwepo kwenye uwanja wa michezo au kuangalia kwenye TV … Je! unaweza ukafikiria sana kuhusu kazi ngumu ya mazoezi ya masaa mengi huku wakijinyima vitu vingi ili kufaulu na kupata ushindi? Jibu? Si mara nyingi tunayowaza mambo hayo, bali tunafurahia kuwa mashabiki kati ya wengine tukishangilia wanavyocheza tu.
Lakini bila maumivu na kujinyima ambavyo havionekani ni dhahiri, kwamba wasingeweza kufika hapo. Kumbe! Na ndivyo ilivyo katika hatua za kutembea ki-imani. Usipojitaabisha faraghani, huwezi kudhihirika kwenye uwanja wa mpira.
Yakobo 1:21,22 Kwa hiyo wekeeni mbali uchafu wote na ubaya uzidio, na kupokea kwa upole neno lile lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu. Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu.
Kwa maneno mengine, hata kama wengine wakikuona au la, yote yanaanzia na kupokea kwa upole Neno la Mungu moyoni mwako – Neno liwezalo kuiokoa roho yako. Yanaanza na kusudi la moyo wako kumfuata Yesu hata kama uchafu na ubaya unao-onekana kwenye mazingira yako ungekudhihaki kwa sababu ya maamuzi yako.
Halafu kinachofuata … ni kujitaabisha kwa kujizoeza, kujinyima, kuwa mtiifu, na kuwa mnyenyekevu dhidi ya uovu uliopo mbele yako. Mwanariadha angeweza kusoma vitabu vingi tu kuhusu mchezo wake alieuchagua, lakini haiwezi kumsaidia kufaulu kuingia kwenye uwanja wa mchezo. Lazima atoke nje na kuanza kufanya mazoezi.
Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.