Imani na Wema
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
2 Petro 1:3,5 Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe ... Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa.
Acha nikuulize, Mtu ataanzaje kujenga maisha bora? Maisha tele yanayoridhisha? Maisha yanayotikisa watu wengine kwa kuwaletea mema? Atatumia hatua gani?
Siyo swali la kinadharia tu, hata kidogo. Kila mtu anapewa kuishi hapa duniani mara moja tu, na maisha hua yanapita haraka. Ndiyo maana leo na katika wiki inayokuja, tutachukua muda wakutafakari kwa pamoja jinsi tunavyoweza kujenga maisha bora.
2 Petro 1:3,5 Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe … Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa.
Ina maana, kwa kupitia Yesu, kama tulishamwamini, tayari Mungu ameshatukirimia uwezo kwa kuishi maisha bora. Kwa kweli, badala ya kujitahidi kujipanga vizuri sisi wenyewe, tayari ameshatupa kila kitu kinachohitajika kwa kuishi maisha ya kujitolea kwake. Sasa muda umewadia kushirikiana naye ili maisha yetu yabadilike.
Leo hii, tuamini ukweli huo. Tuamini kwamba yale anayotwambia ni hakika. Amini kwamba Yesu ni yule yule ambaye anajidai kuwa. Amini kwamba Mungu anataka kutikisa maisha yake akuletee mema. Najua kwamba kuna siku hatujisikii kuwa wema wala hatutendei mema!
Lakini kama umeanza kumwamni Yesu, tayari ameshakupa vyote vinavyohitajika. Kwa hiyo utie wema katika imani yako … na utakuwa umeanza vizuri.
NA Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.