Inapokuwa Vigumu Kumpenda Mtu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mathayo 5:43-45 Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako; lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.
Mara kwa mara tunakutana na watu wanasumbufu kweli, wanaotukwaza, wanatudhalilisha na kutuudhi. Hatupendi lakini hatuna budi kukutana nao. Sasa mtu anakabilianaje na watu kama hao?
Kuna wengine wetu kwa asili ni wepesi wa kuumia kuliko wengine. Mimi niko tofauti, siumii kwa haraka. Lakini wengine, kama vile mke wangu mrembo, ni mpole na anahisia za kuathirika kwa haraka. Sikiliza sasa, haijalishi unasili gani, itafikia mahala watu wakorofi watajaribu kukuumiza kwa vyovyote vile.
Kwanini hawawezi kuwa kama wale wengine wema unaofahamu? Kwanini wanatafuta kujenga uadui? Utafanyaje ili uweze kukabiliana nao?
Mathayo 5:43-45 Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako; lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.
Mara nyingi tunataka kuwachukia adui, kujilipiza kisasi moja kwa moja au kutumia mbini za chini-chini. Tunataka kuwatenga na kuwaadhibu … huu ni muitikio wa kawaida wa mwanadamu.
Lakini Yesu alitufundisha tofauti kabisa. Alitufundisha kuwaombea. Hii inaenda kinyume cha msimamo, sindiyo? Lakini … mtapata kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni.
Waombee adui zako .
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.