... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Stahamala

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Waefeso 4:2 Kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo.

Listen to the radio broadcast of

Stahamala


Download audio file

Laiti watu wote wa ulimwenguni wangekubaliana nasisi, Laiti wangekuwa na mtazamo kama wetu … yaani ingekuwa ajabu kweli, Amani. Maelewano.  Siku zenye furaha.  Hadi raha!

Miezi hii michache tumekuwa tukiongelea kuhusu mada hii, na kwasababu ya kutokuelewana; hii inshu imekuwa ngumu.  Kwanza, kuna mambo mengi tusiyoweza kukubaliana nayo. Pili, kwa kuwa teknolojia imepiga hatua sana, kuna maeneo mengi yakukosa maafikiano. 

Huwa najiuliza, hivi, wazee wetu wa zamani na viongozi maarufu wangefanya nini kwenye kuona maandamano au kurushiana kwa maneno makali mtandaoni, watu kama Winston Churchill, Mahatma Gandhi, Abraham Lincoln na wengine wanaofanana nao. 

Je!, Wangeendelea kuwa maarufu au wangekomeshwa na umati wa watu kwenye mtandao?.  Hatuwezi kujua, Tunachokijua ni sisi ni kwamba ulimwengu wetu unazidi kukosa uvumilivu na ustahimilivu,  tena istoshe, watu wamefafanua neno, “ustahilivu” visivyo kabisa.  Yani wao wanafikiri ustahimilivu ni ni kukubali oni fulani la mtu mwingine ambalo hakubaliani nalo, hapana.  Ustahimilivu ni vile tunavyomtendea mtu asiyekubaliana nasi hata kidogo, huku tukimstahi kwa unyenyekevu na upendo. Hili ndilo lengo la Mungu: 

Waefeso 4:2  Kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo. 

Ni lini tunapaswa kuwa wanyenyekevu na wapole?  Ni siku zote, tuwe wavumilivu kwa akina nani?, Ni kila mtu bila kumwacha hata mmoja.  Hakuna kukwepa wajibu wetu. 

Mungu anafahamu kwamba maoni ya watu wengine yanatusumbua na kutuchanganya.  Si kwamba tunapaswa kukubaliana nao.  Lakini inabidi tuwapende kwa uvumilivu, unyenyekevu na upole. 

Ebu fikiria dunia yetu ingekuaje kama tungetekeleza masharti hayo! 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.