Injili Yenye Ukinzani
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mithali 12:27 Mtu mvivu hapiki mawindo yake; bali mwenye bidii anazo mali za thamani.
Kwa kweli, kuna wakati habari njema hii of Yesu inasikika kama si habari njema hata kidogo. Kwa kuwa yeye mwenyewe aliahidi kwamba kuwa mwanafunzi wake kutakuwa kazi ngumu. Je! Hii itakuwa habari njema kweli?
Kuna wakati utajikuta unapambana na majaribu kwa jinsi wasioamini wasingeweza kamwe kupambana nayo. Bali wao watakutesa. Halafu agizo la Yesu kuwapenda wanaotutesa (!) kama vile tunajipenda sisi wenyewe … jamani, ni usumbufu mtupu.
Jana tuliangalia jinsi Mungu alivyokabiliana na dhambi zetu kwa kuziweka mabegani mwa Yesu, ili wakati tunamwamini, tunapewa msimamo bora kuwa wenye haki mbele zake kama zawadi tu.
2 Wakorintho 5:21 Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye.
Zawadi kubwa sana bila malipo pamoja na thawabu zinazoendelea milele daima. Lakini Yesu aliahidi kwamba safari itakuwa ngumu. Pamoja na hayo, tunafahamu kwa kuwa sisi wenyewe tumeshaona kwamba sio rahisi kupiga hatua maishani bila kuwa na juhudi.
Mithali 12:27 Mtu mvivu hapiki mawindo yake; bali mwenye bidii anazo mali za thamani.
Kwa upande mmoja kuna karama bure ya neema na kwa upande wa pili kuna kazi ngumu. Si ukinzani? Mimi sijui, lakini ninaweza kukwambia tu yafuatayo:
Wakati mtu anaanza safari hii, anaanza upya kabisa akiishafutiwa makosa yake yote. Kwa kweli, njiani atakumbana na majaribu mazito, lakini kupitia majaribu haya, Yesu anambadilisha kuwa mtu mpya, yule ambaye aliyekusudiwa awe.
Kumbe! Ukinzani huu umekuwa sasa ushirikiano unaopendeza sana katika safari yetu kwenda mbinguni.
Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.