Je! Imani Ina Umuhimu Gani?
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Waebrania 11:6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.
Tunahitaji imani halisi katika mapambano tunayokutana nayo maishani. Imani iliyo hai. Imani inayojitokeza kipindi kigumu. Imani inayotusaidia kushinda ulimwengu.
Je! Umewahi kuwaza kwa nini iwe hivyo? Kwa nini Mungu alipanga iwe hivyo badala ya kutuonekania mara moja na kutusaidia kuepukana na majaribu na mateso. Lakini sasa anataka tuonyeshe imani kwake yeye Mungu asiyeonekana kwa macho, asiyeguswa, Mungu ambaye hatumsikii kwa sauti. Kwa nini Mungu anadai tuwe na imani?
Kama Mungu angeonekana wazi na kufikiwa mara moja, kama angetuonekania na kuingilia kati kila wakati ili azuie maumivu na mateso yote tusisumbuke kamwe, ingekuaje? Ebu fikiria mzazi ambaye angetenda hivyo? Watoto wake wote wangekulia katika mazingira yasiyo na nidhamu na hatimaye wangekuwa watundu na watovu wa nidhamu, si kweli?
Bali Mungu, kama mzazi mwema, anawapa watoto wake fursa ya kuchagua wenyewe kumfuata au la, kufanya maamuzi sahihi au la, kumtegemea au la.
Waebrania 11:6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.
Sikiliza vizuri. Mungu anajishughulisha na kazi ya kukuza imani yako kwake na kwa kufanya hivyo, anastawisha tabia yako ndani yake. Sasa shida ikija, chukua fursa kuamini moyoni mwako kwamba yupo kabisa pia kwamba anawapa thawabu wale wamtafutao.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.