Je! Ninahitaji Kuokolewa Kweli Kweli?
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
2 Timotheo 1:10 Na sasa inadhihirishwa kwa kufunuliwa kwake Mwokozi wetu Kristo Yesu; aliyebatili mauti, na kuufunua uzima na kutokuharibika, kwa ile Injili.
Baada ya siku chache, tutasherehekea Krismasi – ujio wa Mwokozi wetu ulimwenguni mwetu. Lakini inabidi tuulize swali, swali ambalo wengi wanajiuliza, Je!, Kweli ninahitaji kuokolewa?
Hivi karibuni nilikuwa ninaongea na mama mmoja mzee na hatimaye nilimuuliza, “Je!, Unafikiri itakuaje siku utakapokufa?” Alinijibu kwa wasiwasi kwa kusema hivi …
Sina uhakika kwamba nimeishi maisha vizuri yakunitosha kuingia mbinguni. Labda nimestahili au pengine sikustahili. Ninatumaini labda …
Jibu lake lilinishtua, kwahiyo niliweza kumwambia ukweli ufuatao wenye nguvu:
2 Timotheo 1:10 Na sasa inadhihirishwa kwa kufunuliwa kwake Mwokozi wetu Kristo Yesu; aliyebatili mauti, na kuufunua uzima na kutokuharibika, kwa ile Injili.
Yesu – ambaye anatajwa mara nyingi kuwa Mwokozi wetu – alikuja kufanya nini? Kubatili mauti, na kuufunua uzima na kutokuharibika.
Nisikilize vizuri. Mungu hana munzani wa haki mikononi mwake ili apime mema yako kwa kuyalinganisha na mabaya yako aone uzito utaelekea upande gani,
Badala ya kufanya hivyo, alimtuma Mwanae Yesu – na hili ndilo lengo la Krismas – ili aweze kubeba “mabaya” yako mabegani mwake wakati aliadhibiwa kwaajili yako pale msalabani, ili kwamba ukimwamini yeye, utakuwa na karama bure ya uzima wa milele. Unahitaji kufanya nini? Nikuaamini tu … Yesu alikuja kufa kifo chako na kuufunua uzima wa kutokuharibika.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.