... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Hayo Siyo Niliyotaka Kuyasikia

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mathayo 21:33-38 Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu mwenye nyumba, naye alipanda shamba la mizabibu, akalizungusha ugo, akachimba shimo la shinikizo ndani yake, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri. Wakati wa matunda ulipokuwa karibu, akawatuma watumwa wake kwa wale wakulima, wapokee matunda yake. Wale wakulima wakawakamata watumwa wake, huyu wakampiga, na huyu wakamwua, na huyu wakampiga kwa mawe. Akawatuma tena watumwa wengine wengi kuliko wa kwanza wakawatenda vile vile. Mwishowe akamtuma mwanawe kwao, akisema, Watamstahi mwanangu. Lakini wale wakulima walipomwona yule mwana, wakasemezana wao kwa wao, Huyu ni mrithi; haya na tumwue, tuutwae urithi wake.

Listen to the radio broadcast of

Hayo Siyo Niliyotaka Kuyasikia

Download audio file

Leo ninataka kukushirikisha mfano Yesu alioutoa. Lakini kabla hatujauchunguza, kumbuka hili: Mara nyingi Mungu huwa anatwambia maneno ambayo hatutaki kuyasikia. Upendo wake ni upendo mkali kwasababu alikuja kutuweka huru na dhambi inayotufunga.

Sasa, sikiliza mfano niliokwambia: 

Mathayo 21:33-38  Sikilizeni mfano mwingine.  Kulikuwa na mtu mwenye nyumba, naye alipanda shamba la mizabibu, akalizungusha ugo, akachimba shimo la shinikizo ndani yake, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri.  Wakati wa matunda ulipokuwa karibu, akawatuma watumwa wake kwa wale wakulima, wapokee matunda yake.  Wale wakulima wakawakamata watumwa wake, huyu wakampiga, na huyu wakamwua, na huyu wakampiga kwa mawe.  Akawatuma tena watumwa wengine wengi kuliko wa kwanza wakawatenda vile vile.  Mwishowe akamtuma mwanawe kwao, akisema, Watamstahi mwanangu.  Lakini wale wakulima walipomwona yule mwana, wakasemezana wao kwa wao, Huyu ni mrithi; haya na tumwue, tuutwae urithi wake. 

Yesu mwenyewe ndiye mwana katika mfano ule.  Alikabiliana moja kwa moja na dhambi za watu. Walimchukia kabisa, walifanya asulubiwe. Rafiki yangu, Yesu akikabiliana na dhambi maishani mwako, tafadhali, usimkatalie.  Pokea pendo lake linaweza kuokoa uhai wako. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.