... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Je! Unamwamini Nani au Unakitumaini Kitu Gani?

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Wafilipi 3:2,3 Jihadharini na mbwa, jihadharini na watendao mabaya, jihadharini na wajikatao. Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Mungu kwa Roho, na kuona fahari juu ya Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili.

Listen to the radio broadcast of

Je! Unamwamini Nani au Unakitumaini Kitu Gani?


Download audio file

Kuna kitu kimoja kinachosababisha ninywee kila mara ninaposoma habari ndani ya Biblia. Ni mada yanayohusu tohara.  Ilikuwa masharti kwenye sheria ya Agano la Kale, zamani kabla ya dawa ya nusukaputi tutengenezwa.  Uuwiiii, ahaha, jamani, tohara bila ganzi, ahahaha

Kumtahiri mwanamume kulikuwa dalili kwenye mwili wake kwamba yeye ni mmoja wa watu wa Mungu.  Ilikuwa sharti la sheria chini ya agano tunaloliita Agano la Kale – yaani mapatano kati ya Mungu na watu wake. 

Lakini Kristo alipokuja, alitimiza sheria.  Kanuni zile za zamani na masharti ya sheria hazina tena umuhimu kwa yule aliyeamini sadaka Yesu aliyoitoa pale msalabani ili asamehewe na Mungu badala ya kushika amri 613 zilizoandikwa ndani ya Torati – Mwanzo, Kutoka, Walawi, Hesabu na Kumbukumbu. 

Sasa tumeingia siku za furaha – hususani kwa jamaa kama mimi!  Sasa chini ya Agano Jipya la neema, yote yanahusu muitiko wetu kwa yale Yesu aliyotutendea badala ya sisi kushika sheria, kitu ambacho hakuna awezaye kuishika kikamilifu. 

Lakini … bado kuna watu wanasisitiza kwamba turidie Agano la Kale.  Yafuatayo ni yale Mtume Paulo alisema kuhusu watu kama hawa: 

Wafilipi 3:2,3  Jihadharini na mbwa, jihadharini na watendao mabaya, jihadharini na wajikatao.  Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Mungu kwa Roho, na kuona fahari juu ya Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili. 

Ni maneno makali kweli.  Anachokilenga hapa ni kuonyesha kwamba ibada ya kweli ni kumwabudu Mungu kwa Roho, badala ya kupitia njia za kanuni na masharti.

Usitapanye uhuru wako kwa kurudia tena sheria inayojengwa juu ya masharti.  Yesu alikuja kukuweka huru, rafiki yangu.  Sasa uko chini ya neema yake, hauko tena chini ya sheria. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy