Je!, Watu Wanaweza Kukuamini?
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mithali 28:19,20 Alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele; bali afuataye mambo ya upuzi atapata umaskini wa kumtosha. Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele; lakini afanyaye haraka kuwa tajiri hakosi ataadhibiwa.
Swali ninalokwenda kukuuliza labda litakusumbua, Je!,Wewe ni mwaminifu? Au tuulize swali lingine ambalo yamkini ni muhimu zaidi, je! Familia yako inaweza kukuamini?, Wanaweza kukutegemea? Upo kwa ajili yao au uko bize kiasi kwamba huwajali tena?
Kosa kubwa nililolifanya katika maisha yangu ni kuwa bize kiasi cha kutokujali familia yangu; kulenga tu namna ya kupanda cheo kazini; kupata pesa zaidi; kuwa bize na kupuuza mambo ya kila siku ya familia yangu. Ilinigharimu kabisa na kuvunja ndoa yangu ya kwanza. Ilisababisha majonzi makubwa kwa watoto wangu.
Kwanini nakwambia haya? Ni kwasababu watu wengi wanaume kwa wanawake huwa wanakuwa bize sana wanapotaka kufanikisha kufanikisha mambo yao katika ulimwengu huu wasiwekeze lolote kwa watu waliopaswa kuwathamini kuliko wote duniani – yaani familia zao.
Kwaufupi tu, hawaaminiki tena kama mume au mke, kama baba au mama, kama mwana au binti … ambaye Mungu amekusudia wawe. Hiki, ninachokwambia, ndicho kinachotenganisha familia kabisa.
Mithali 28:20 Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele; lakini afanyaye haraka kuwa tajiri hakosi ataadhibiwa.
Usinielewe vibaya, kufanya kazi kwa juhudi ni jambo jema. Mstari uliotangulia mstari huo unasema hivi:
Mithali 28:19 Alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele; bali afuataye mambo ya upuzi atapata umaskini wa kumtosha
Lakini wakati kazi na mali vinaanza kupata kipaumbele kwetu, familia zetu hazitaweza kutuamini tena. Mwanaume au mwanamke afanyaye haraka kuwa tajiri atakosa baraka za upendo wa familia na atakula hasara mwenyewe.
Usiwe mtu kama huyo wewe baba. Usiwe mwanamke kama huyo wewe mama.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.