... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Jiepushe na Tabia Hii Mbaya

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Waebrania 10:23-25 Na mlishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke; maana yeye aliyeahidi ni mwaminifu; tukaangaliane sisi kwa sisi na kuhimizana katika upendo na kazi nzuri; wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.

Listen to the radio broadcast of

Jiepushe na Tabia Hii Mbaya


Download audio file

Pale wewe na mimi tunapoweka tegemeo letu ndani ya sisi wenyewe, au ndani ya vipaji vyetu, tunaweza kujiamini kupita kiasi. Lakini mtu anapomtegemea Mungu, kwa kweli hawezi kumwamini kupita kiasi.

Kama tulivyoona jana, tunaweza kushika ungamo la tumaini letu ndani ya Mungu kwa sababu … Yeye ni mwaminifu daima.  Kamwe hawezi, hawezi kabisa kukuangusha. Ni habari njema mno, hususani pale imani yako inapoyumba. 

Lakini kufanya hivyo na kushika tumani lako kwa Mungu peke yako sio rahisi, hata kwa yule mwenye nguvu na juhudi kati yetu.  Kwa hiyo … 

Waebrania 10:23-25  Na mlishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke; maana yeye aliyeahidi ni mwaminifu; tukaangaliane sisi kwa sisi na kuhimizana katika upendo na kazi nzuri; wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia. 

Imani yetu na tegemeo letu kwa Mungu ni kama misuli kwenye mwili.  Lazima misuli izoezwe ili iendelee kuwa na nguvu. Ndiyo maana kukaa na waamini wenzetu, kupendana na kuhudumiana na kukusanyika pamoja ni tabia nzuri iletayo nguvu. 

Sasa kushindwa kufanya hivyo ni tabia mbaya mno kwa sababu Mungu alitufanya tuwe familia sehemu ambayo kama ndugu ndani ya Kristo tunategemezana, tunahudumiana na tunatiana moyo. Ndio njia uwezayo kubaki imara katika imani yako. Njia hiyo inaitwa “kanisa” – hata kama kuna mifumo mbalimbali ya namna tunavyokuwa kwa pamoja, mwili wa Kristo. 

Kwahiyo, hata mkusanyikaje kama “kanisa” …  tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy