... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Ulishike Sana Ungamo Lako

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Waebrania 10:23 Na mlishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke; maana yeye aliyeahidi ni mwaminifu.

Listen to the radio broadcast of

Ulishike Sana Ungamo Lako


Download audio file

Kwa mtazamo nilio nao mimi, hakuna kazi nzuri kama kuwa mtu anayepeleka habari njema.  Na leo si kwamba nina habari njema kwa ajili yako, yaani nina habari njema mno. Dua yangu ni kwamba uwe tayari kuipokea moyoni mwako.

Kama nilivyoeleza wiki iliyopita, msikilizaji wetu mmoja aliomba msaada kwa ajili ya imani yake iliyokuwa inafifia ili iwe imara daima. Kwa hiyo, kwa siku hizi chache ndivyo tulivyokuwa tunavyofanya kwa pamoja. Kufungua Neno la Mungu na kumruhusu Yeye alete jibu kwa hali kama hiyo. 

Kwasababu huwa inatutokea sisi sote mara kwa mara kuona imani yetu inapungua.  Kwa hiyo tuendelee kuchunguza mstari unaofuata, ujumbe unaofuata, hatua inayofuata kwa kumruhusu Mungu aimarishe imani yetu. 

Waebrania 10:23  Na mlishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke; maana yeye aliyeahidi ni mwaminifu. 

Kushika tumaini na kuliungama, na kulikiri kwa ujasiri wakati mambo yanakatisha tamaa kabisa – ni rahisi kusema hivi lakini ni vigumu mno kutekeleza isipokuwa uwe na sababu za msingi kuungama hivyo. Na hapa hapa kwa mstari huu, Mungu anakupa sababu hiyo.  Chunguza tena … Na mlishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke; maana yeye aliyeahidi ni mwaminifu.  

Kwa nini unaweza kulishika tumaini hilo?  Kwanini unaweza kuliungama?  Kwa nini unaweza kufanya hivyo bila kusitasita?  Ni kwa sababu Mungu aahidiye ni mwaminifu. Ni mwaminifu kukuosha dhambi zako kupitia dhabihu ya Yesu pale msalabani. Yeye ni mwaminifu kukubeba hadi mwisho. 

Kwahiyo, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu nakwambia, Ulishike sana ungamo la tumaini lako lisigeuke. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.