... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Usiutupe Ujasiri Wako

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Waebrania 10:32-36 Lakini zikumbukeni siku za kwanza, ambazo, mlipokwisha kutiwa nuru, mlistahimili mashindano makubwa ya maumivu; pindi mlipotwezwa kwa mashutumu na dhiki, na pindi mliposhirikiana na wale waliotendewa hayo. Maana mliwaonea huruma wale waliokuwa katika vifungo, tena mkakubali kwa furaha kunyang’anywa mali zenu, mkijua kwamba nafsini mwenu mna mali iilyo njema zaidi, idumuyo. Basi msiutupe ujasiri wenu, kwa maana una thawabu kuu. Maana mnahitajji saburi, ili kwamba mkiisha kuyafanya mapenzi ya Mungu mpate ile ahadi.

Listen to the radio broadcast of

Usiutupe Ujasiri Wako

Download audio file

Kuwa na ujasiri kunaweza kutuletea uwezo katika maisha yetu, ikiwa tunategemea yaliyo sahihi.  Sasa katika mapambano ya maisha haya, acha nikuulize, Una ujasiri kiasi gani?

Kama umemwamini Yesu, nadhani kulikuwa kipindi, labda mapema ulipoanza kumpokea maishani mwako, ambacho ulikuwa na shauku kubwa na ujasiri mkubwa ndani yake.  Ulikuwa na moyo mkuu ukitazamia safari yako iliyokuwa mbele yako.

Lakini pole pole, hali halisi ya maisha yalianza kukulemea.  Kidogo kidogo, kule kusongwa na shughuli za kila siku kulianza kubambua ujasiri uliokuwa umeanza nao.  Kwa kifupi, imani yako ilififia, si kweli?

Habari njema ni kwamba hayo si mambo mapya.  Hauko peke yako na leo, kwa kupitia Roho yake na Neno lake, mimi ninaamini kwamba Mungu atapuliza tena ujasiri wake, urejee moyoni mwako; atakukirimia yale yote unayohitaji.  Je!  Uko tayari kuupokea?

Waebrania 10:32-36  Lakini zikumbukeni siku za kwanza, ambazo, mlipokwisha kutiwa nuru, mlistahimili mashindano makubwa ya maumivu; pindi mlipotwezwa kwa mashutumu na dhiki, na pindi mliposhirikiana na wale waliotendewa hayo.  Maana mliwaonea huruma wale waliokuwa katika vifungo, tena mkakubali kwa furaha kunyang’anywa mali zenu, mkijua kwamba nafsini mwenu mna mali iilyo njema zaidi, idumuyo.  Basi msiutupe ujasiri wenu, kwa maana una thawabu kuu.  Maana mnahitajji saburi, ili kwamba mkiisha kuyafanya mapenzi ya Mungu mpate ile ahadi.

Kwa uwezo wa Roho Mtakatifu ninakwambia, Usiutupe ujasiri wako kwa maana una thawabu kuu.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.