Jinsi Unavyosafiri
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
2 Timotheo 1:7 Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.
Je! Wewe unasafiri umbali gani kila siku? Labda unaenda kazini kila siku na kurudi nyumbani jioni. Labda unafanya mazoezi ya kutembea au kukimbia. Kuna wakati unaweza kusafiri mbali zaidi. Nijibu, kwa wastani, kila siku unasafiri umbali gani?
Kama ilivyoelezwa katika makala ndani gazeti ya BBC Sayansi, kila siku dunia inatembea kilomita miliyoni 2 na ½ ikizunguka jua, pia inatembea kilomita miliyoni 19 kwa kuzunguka kiini cha kundi letu la nyota iitwayo Galaxi ya Njia ya Maziwa.
Ina maana kwamba wewe pia kila siku unatembea kasi kupitia anga bila kujua, umbali ulitajwa na Hii ndiyo hali halisi ya matembezi yako maishani. Hayo yananiduaaza, sijui wewe?
Kuna kweli nyingine inayoshangaza pia kuhusu safari ya mtu awaye yote anayemwamini Yesu.
2 Timotheo 1:7 Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.
Mungu – Muumba wa Mbingu na Nchi – ameweka Roho yake Mtakatifu kukaa ndani ya mtu awaye yote aliyechagua Yesu kuwa kiini cha maisha yake kwa imani. Sasa tukiwa na uwezo wote ule, upendo wote ule na kujithibiti kote kule – zaidi ya mahitaji yetu, wewe na mimi – ndani ya mioyo yetu, kama kiwanda cha kuzalisha umeme wa kutusukuma mbeleni katika maisha aliyoandaa kwa ajili yetu.
Rafiki yangu, wakati unamtegemea Yesu, hauko peke yako tena. Daima una nguvu, upendo na kiasi ambavyo vitakutosha kupitia majaribu na matatizo yote ya ulimwengu huu.
Kwa hiyo, usiogope. Umepewa kila kitu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.