Jinsi Unavyowatendea Wafanyakazi Wako
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Wakolosai 4:1 Ninyi akina bwana, wapeni watumwa wenu yaliyo haki na ya adili, mkijua ya kuwa ninyi nanyi mna Bwana mbinguni.
Mtu awaye wote aliyekuwa na majukumu ya kuongoza watu wengine anafahamu kwamba ni kazi ngumu. Kuna wakati watu wanakuangusha kabisa. Vile vile, hauna budi kukosolewa.
Kwa kweli, kuwa kiongozi si jambo rahisi. Kama vile Steve Jobs, aliyeanzisha kampuni ya komputa ya Apple aliwahi kusema, kama unataka kumpendeza kila mtu, usijaribu kuwa kiongozi. Nenda kauze mandazi!
Na kwa sababu viongozi hua wanabanwa sana na mambo mengi, mara nyingi wanaweza kuanza kuwatendea wale ambao wanawaongoza vibaya … au kama hawakusudii kuwatendea vibaya, bado wanaweza kuwapuuza, wasisome hisia zao, wasijali mahitaji yao na khadhalika.
Hailishi kama wewe ni kiongozi au la, Neno hili linalotoka kwa Bwana ni muhimu kwako:
Wakolosai 4:1 Ninyi akina bwana, wapeni watumwa wenu yaliyo haki na ya adili, mkijua ya kuwa ninyi nanyi mna Bwana mbinguni.
Yaliyo haki na ya adili. Mtu awaye wote akiwa chini ya uongozi wa mwingine asingeweza kudai zaidi ya hayo. Hata kama ni mimi ninayeongoza huduma ya Christianityworks (yaani Ukristo unafanya kazi kweli kweli) huduma nayoandaa kipindi hiki cha Neno Safi na Lenye Afya, mimi bado niko chini ya uongozi wa bodi inayojitegemea.
Nakwambia, wananibana kutoa mahesabu sahihi. Pia wananihoji maswali magumu kama inavyowapasa. Lakini wanaifanya wakitumia adili na haki.
Hailishi wewe ni kiongozi au la, Kristo anakuagiza kuwa mwadilifu na mwenye haki na wale ambao unaofanya kazi nao – walio chini yako, wanaolingana na wewe, na viongozi wako. Kumbuka kwamba kuna sababu inayoeleweka kabisa!
Mkijua ya kuwa ninyi nanyi mna Bwana mbinguni.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.