... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Jinsi ya Kuwa Adui wa Mungu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yakobo 4:4-6 Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu. Au mwadhani ya kwamba maandiko yasema bure? Huyo Roho akaaye ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu? Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajitukuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.

Listen to the radio broadcast of

Jinsi ya Kuwa Adui wa Mungu

Download audio file

Nikubalie kwanza tafadhali, nikuulize swali.  Haijalishi unaamini nini kuhusu uwepo wa Mwenyezi Mungu na wa upendo pia. Kama kweli yupo, je!  Ungependa kuwa adui wake kweli-kweli?  Kuna mtu angetaka kuwa adui wa Mungu?

Kuwa adui wa Mungu!?  Ni dhana inayotisha kabisa.  Lakini hata hivyo, watu wengi sana – hata baadhi ya wanaokiri kwamba wanamwamini Yesu aliyekufa na kulipa deni la dhambi zao kisha akafufuka tena ili awape maisha mapya, uzima wa milele – wengi tayari wameshajifanya kuwa adui, adui wa Mungu mwenyewe. 

Inawezekanaje?  Acha nikuonyeshe: 

Yakobo 4:4-6  Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu?  Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu.  Au mwadhani ya kwamba maandiko yasema bure?  Huyo Roho akaaye ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu?  Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajitukuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu. 

Kadiri tunavyozidi kupenda mambo ya ulimwengu huu – anasa, mali, cheo, kujulikana, maporomoko ya maadili, usokotaji wa uongo – ndivyo tutavyosonga mbele kuingia ndani ya eneo lenye hatari ya kuwa adui wa Mungu. Usibishe, ni rahisi sana kuelekea upande ule siku hizi katika ulimwengu wetu wa kisasa, si kweli? 

Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajitukuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.  

Ebu fikiria … ingekuaje kama ungejishusha na kuachana na kiburi cha ulimwengu huu na kuwa mwaminifu kwa Mungu? 

Kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.