... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kuokolewa na Mkono wa Wasio Haki

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 97:10-12 Enyi mmpendao BWANA, uchukieni uovu; huwalinda nafsi zao watauwa wake, na kwaokoa na mkono wa wasio haki. Nuru imemzukia mwenye haki, na furaha wanyofu wa moyo. Enyi wenye haki, mfurahieni BWANA, na kulishukuru jina lake takatifu.

Listen to the radio broadcast of

Kuokolewa na Mkono wa Wasio Haki


Download audio file

Je!, Na wewe huchukii wakati wasio haki wanapata ushindi dhidi yako?  linamtikisa mtu kwa ndani kabisa, ina leta maswali, “Mungu!  Unafanya nini?  Kwanini unaruhusu hayo yanipate?”

Nina rafiki wa karibu ambaye amefaulu vizuri katika biashara yake na kwa hiyo amekusanya mali nyingi. Sasa mtu angefanyaje na pesa zile nyingi?  Kama kweli unamwamini Yesu, utazitoa kwaajili ya kazi yake ya kuokoa ulimwengu huu na dhambi zao. 

Sasa wakati rafiki yangu anaanza kufuata mstari huo, kundi la watu waliojikusanya kumfungulia mashtaka ya madai, si kwamba aliwakosea, bali ni kwasababu walifikiri wamepata fursa ya kula pesa za udhalimu. 

Ile kesi iliendelea muda mrefu na aliumia sana na kuhangaika hadi pale alipoweza kuafikiana na kumaliza kesi … maana yake ilimbidi abebe kiasi kikubwa cha pesa ambazo alikuwa amezitengea kwa ajili ya kazi ya Bwana. 

Uonevu kama huo unaweza kutupata sisi sote hata kama si kwa kiwango kikubwa kama hicho.  Sasa Mungu unafanya nini?!

Zaburi 97:10-12  Enyi mmpendao BWANA, uchukieni uovu; huwalinda nafsi zao watauwa wake, na kwaokoa na mkono wa wasio haki.  Nuru imemzukia mwenye haki, na furaha wanyofu wa moyo.  Enyi wenye haki, mfurahieni BWANA, na kulishukuru jina lake takatifu. 

Si kwamba mstari huu daima utasababisha tusidhulumiwe. Lakini kama unatendewa visivyo haki, jua hili.  Bwana atakukokoa na mkono wa wasio haki.  Nuru itakuzukia na furaha itajaa moyo wako.  Shikilia ahadi hiyo.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.