Kanyaga Njia Iliyo Sahihi
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mithali 12:28 Katika njia ya haki kuna uhai; wala hakuna mauti katika mapito yake.
Safari ya maisha ina makona mengi na ina njia panda nyingi pia. Bila shaka, ukiangalia nyuma, unaweza kuona jinsi maamuzi madogo kwenda huku badala ya kwenda huko, yaliweza kubadilisha kabisa mwelekeo wa maisha yako.
Zamani, wakati nilikuwa nimegeuka kuwa Mkristo punde tu kama vile dakika tano, niliona kama kwa bahati nasibu, jengo dogo lisilovutia la kanisa. Kwa hiyo niliamua tu kuhudhuria pale Jumapili iliyofuata.
Nilikuwa bado na mtazamo mkali na moyo mgumu, kwa hiyo niliona kwamba hata kwa ndani, hapavutii. Lakini kupitia washirika wale wazuri sana, Mungu alibadilisha maisha yangu kabisa. Jumapili fulani niliona rosha ya chuo cha Biblia iliyokuwa karibu na kwetu na niliamua kusomea digrii ihusuyo huduma ya kikristo, hata kama nilikuwa Mristo mchanga tu.
Sasa tuko pamoja wewe na mimi, baada ya miaka mingi nikiwa na fursa ya kukushirikisha kwa Habari Njema ya Yesu. Ebu angalia, maamuzi madogo mawili lakini angalia sasa matokeo na mahali nilipofikia!
Maamuzi yale, sikuyajadili. Ni kama nilifuata silika yangu tu. Lakini mtu ataamuaje akifika kwenye njia panda? Kila mtu hana budi kufanya maamuzi ili apitie njia iliyo sahihi hapo kwenye njia panda.
Mithali 12:28 Katika njia ya haki kuna uhai; wala hakuna mauti katika mapito yake.
Daima uchague njia ya haki. Kadiri unavyozidi kumfuata Yesu, ndipo dhana ya haki kama vile inavyoelezwa katika lugha ya asili ya Kiebrania, itakuongoza bila wewe kufikiria sana. Kumfuata Yesu ni kama mafunzo mtu anapata kazini yanayomwonyesha wema na haki vinafananaje.
Katika njia ya haki kuna uhai; wala hakuna mauti katika mapito yake.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.