Kila Upigayo Hatua
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mithali 3:6 Katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyosha mapito yako.
Ni rahisi sana kusema kwamba utamtegemea Mungu wakati wa shida. Lakini utekelezaji wake sio rahisi na ni kwasababu Mungu haonekanikwa macho.
Huduma ninayoshughulika nayo inayoandaa vipindi hivi vya Neno la Mungu kila siku inaitwa Christianityworks, yaani Ukristo Unatenda Kazi. Kwa nini jina hilo? Ni kwasababu ninaamini kwa moyo wangu wote, tena nina uhakika ya kwamba ukristo unatenda kazi kweli kweli. Kumfuata Yesu kunaleta matokeo ya uhakika. Kumtegemea Yesu ni amina kabisa.
Na kama ni hivyo, lazima Ukristo “utende kazi” vipindi vyote vizuri kwa vibaya. Sasa tuzungumze kidogo kuhusu vipindi vigumu, Je! inakuwia rahisi (au la) kumtegemea Yesu wakati unakabiliana na mazingira magumu sana? Hmm?
Tunajua kama inatupasa kumuamini daima, lakini swali ni hili … Je! Mtu afanyeje? Tunawezaje kumtegemea ki-utendaji? Mtu anawezaje kumtegemea Yesu katika kipindi kigumu?
Mithali 3:6 Katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyosha mapito yako.
Hapo ndipo tunapopata jibu la swali letu, Je! Mtu “afanyaje sasa?” Mstari huu unapatikana katikati ya mistari inayosimulia swala la kumtegemea Mungu katika kipindi kigumu. mtu anapotembea hatua kwa hatua, mara anaumia, mara amekatishwa tama, mara amejaribiwa kutenda yasiyofaa, afanye nini sasa kwa kila hatua??
Katika njia zako zote mkiri yeye. Hii ndiyo njia ya kumtegemea Yesu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.