... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kuokolewa Kutoka kwenye Kinywa cha Simba

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

2 Timotheo 4:17,18 Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu, ili kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, hata wasikie Mataifa yote; nami nikaokolewa katika kinywa cha simba. Bwana ataniokoa na kila neno baya, na kunihifadhi hata nifike ufalme wake wa mbinguni. Utukufu una Yeye milele na milele. Amina.

Listen to the radio broadcast of

Kuokolewa Kutoka kwenye Kinywa cha Simba

Download audio file

Kuna vipindi mambo huwa yanaenda shwari, Halafu kuna vipindi vingine mambo yote huwa yanatuharibikia  sasa hapo ndipo huwa tunatamani Mungu aje atuokoe.

Ni lini uliwahi kupitia kipindi kigumu kama hicho?  Kweli ulikuwa hatarini.  Ulihitaji kabisa Mungu akuonekanie na kuingilia kati kimiujiza; akuokoe au aokoe mpendwa wako katika kinywa cha simba.  Kwa hiyo uliomba na kuomba na kuomba … na kuna nyakati Mungu anakuonekania, lakini pia kuna nyakati huwa haonekani kabisa. 

Kuna wakati Mungu anamponya mpendwa Yule mgonjwa na kuna wakati Mungu huwa anamwacha afe.  Ni kama bahati nasibu,  ni kama mchezo w akamari hivi.  Hali hiyo haiwezi kututia moyo, sidhani.  Je!  Ndivyo mambo yanatakiwa yaende?  Sikiliza mzee Mtume Paulo alivyomwandikia mwanafunzi wake Timotheo kwa kutumia hekima yake:

2 Timotheo 4:17,18  Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu, ili kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, hata wasikie Mataifa yote; nami nikaokolewa katika kinywa cha simba.  Bwana ataniokoa na kila neno baya, na kunihifadhi hata nifike ufalme wake wa mbinguni.  Utukufu una Yeye milele na milele.  Amina. 

Je!, anataka kusema nini katika mistari hiyo?  Kwa kweli, Mungu aliingilia kati mara nyingi kwa ajili ya kumwokoa Paulo.  Ni kwanini?  Ni kwa sababu Mungu alikuwa na makusudi kwa ajili yake, atangaze Injili yenye nguvu ya kubadilisha mataifa.  Lakini huduma yake isingeendelea milele,  Paulo alielewa hilo.  Ndiyo maana alimtegemea Mungu kwamba atamfikisha salama salamini katika Ufalme wake wa Mbinguni. 

Umtegemee Mungu.  Anajua anachokifanya. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.