... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kazia Macho Tuzo

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Wakorintho 9:24-27 Je! Hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, ili mpate. Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji isiyoharibika. Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa; bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.

Listen to the radio broadcast of

Kazia Macho Tuzo

Download audio file

Mimi si mchezaji mzuri ingawa ninapenda kuangalia wachezaji mbalimbali.  Mwezi wa Januari mwaka huu binti mmoja aitwaye Ash Barty, alikuwa Mwaustralia wa kwanza kushinda tuzo kwenye Mashindano Makubwa ya tennis nchini kwetu Australia baada ya miaka 44.

Hautashangaa kusikia kwamba wananchi wote walishangilia pale binti alipoinua kombe aliloshida,  Ni mchezaji mwenye adabu akicheza, tena mnyenyekevu; hajidai wala hana kiburi na unafiki. Lakini anapocheza, jamani, sijaona mtu anayekaza macho akifatilia mpira wa tennis kama yule binti mwenye umri wa 25 tu. 

1 Wakorintho 9:24-27  Je!  Hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja?  Pigeni mbio namna hiyo, ili mpate.  Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji isiyoharibika.  Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa; bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa. 

Si kila mtu anaweza kushinda kombe kwenye mashindano makubwa. Kwa mimi ndo sitaweza kabisaaa,  Lakini, bado kuna tuzo kubwa zaidi inatungojea kama tumeweka imani zetu ndani ya Yesu.  Lakini mtu hawezi kushinda tuzo hiyo idumuyo milele kwa kuzurura tu bila mwelekeo.

Kaza macho.  Usiyaondoe kwenye tuzo iliyombele yako. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.