Kilio cha Kuomba Msaada
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Zaburi 61:1-4 Ee Mungu, ukisikie kilio changu, uyasikilize maombi yangu. Toka mwisho wa nchi nitakulilia nikizimia moyo, uniongoze juu ya mwamba nisioweza kuupanda. Kwa maana ulikuwa kimbilio langu, ngome yenye nguvu adui asinipate. Nitakaa katika hema yako milele, nitaikimbilia sitara ya mbawa zako.
Kazi mojawapo ya mzazi ni kulinda watoto wake. Na mimi kama mme, baba na sasa babu, ni wajibu ambao ninakubali kwa dhati kabisa. Sasa kwa nini mtu angefikiri kwamba Mungu angekuwa tofauti katika swala hilo?
Juzi tuliongea habari ya maisha kuwa na mabonde na milima. matatizo tunayoyapata yanageuka kuwa msiba mkubwa. Sikiliza maneno ya mtu aliyeniomba juzi nimkumbuke katika maombezi:
Nimeshindwa kwenda kazini kwa sababu ya fadhaa na kukatishwa tamaa. Ninahangaika kweli kiuchumi na yote ninayoyafanya yanafeli tu. Nimeshindwa kukidhi mahitaji ya watoto wangu kwa ajili ya masomo; kununua rimu ya kartasi, sare na ada.
Kawaida, matatizo hua yanatujia kwa njia mbali mbali, mengine makubwa, mengine ya wastani. Kwa hiyo nilipenda leo tuchunguze zaidi kwa kutafiti tunafanyaje wakati tumefika chini kabisa na kujikuta tuna hali duni mno.
Zaburi 61:1-4 Ee Mungu, ukisikie kilio changu, uyasikilize maombi yangu. Toka mwisho wa nchi nitakulilia nikizimia moyo, uniongoze juu ya mwamba nisioweza kuupanda. Kwa maana ulikuwa kimbilio langu, ngome yenye nguvu adui asinipate. Nitakaa katika hema yako milele, nitaikimbilia sitara ya mbawa zako.
Mfalme Daudi aliyeandika dua lile, alikuwa mfalme mkubwa katika Israeli kuliko wote hadi pale mfalme mwingine wa aina tofauti kabisa aitwaye Yesu alionekana baada ya miaka elfu moja. Lakini mfalme huu Daudi aliyekuwa hodari katika vita anamlilia Mungu akakiri … Nimezimia moyo!
Halafu, rafiki yangu, acha nikwambie kwamba dua hilo, kama lilimfaa shujaa kama Daudi, basi itatufaa watu kama sisi, wewe na mimi. Mungu wako ni mlinzi wako. Upaze sauti ukamlilie kwa sababu yeye anawajibika sana na kazi hiyo ya kukulinda.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.