... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Krismasi Imekaribia

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Isaya 7:13,14 Naye akasema, Sikilizeni sasa, enyi nyumba ya Daudi; Je! Ni neno dogo kwenu kuwachosha wanadamu, hata mkataka kumchosha Mungu wangu pia? Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli.

Listen to the radio broadcast of

Krismasi Imekaribia


Download audio file

Kumbe!  Imebaki siku kumi tusherehekee Krismasi.  Siku kumi tu!  Mwaka wetu huu umeenda wapi?  Muda umepita kasi.  Nadhani kadiri mtu anazeheka, ndipo mwendo wa muda unazidi kumshangaza.

Makarne kabla ya kuzaliwa kwake Yesu kwenye hori ya mifugo pale Bethlehemu, taifa teule la Mungu, yaani Israel, walikuwa wanatenda mabaya mara kwa mara.  Walikuwa wanabadilikabadilika, mara kumheshimu Mungu, mara kuabudu sanamu wakisahau ni nani aliyewatoa utumwani Misri.  Hata jina lile “Israel” maana yake halisi ni “anayepambana na Mungu.”

Lakini hata hivi, katikati ya maasi yale, Mungu aliwaletea unabii wenye nguvu, matumaini kuhusu hatima itakayokuwa tofauti kabisa. 

Isaya 7:13,14  Naye akasema, Sikilizeni sasa, enyi nyumba ya Daudi; Je!  Ni neno dogo kwenu kuwachosha wanadamu, hata mkataka kumchosha Mungu wangu pia?  Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara.  Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli.  (Maana yake, Mungu pamoja nasi)

Hapo, Mungu anatabiri siku zijazo ambapo hataadhibu watu wake kwa ajili ya dhambi zao, bali ataruhusu adhabu tunayostahili sisi kuanguka juu ya mabega ya Yesu, Mwanae pekee, yeye atakayekufa kulipa deni la dhambi zetu.

Bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake … Mungu pamoja nasi.  Rafiki yangu, siku zile zilizotabiriwa zimeshafika.  Tayari Yesu amekuja kukuweka huru.  Ndiyo maana tunasherehekea Krismasi kwa shangwe kuu.

Yesu.  Alikuja kwa ajili yako.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy