... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kuachana kwa Talaka (3)

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Wakorintho 7:15 Lakini yule asiyeamini akiondoka, na aondoke. Hapo huyo ndugu mume au nduge mke hafungiki. Lakini Mungu ametuita katika amani.

Listen to the radio broadcast of

Kuachana kwa Talaka (3)


Download audio file

Swali lililopo ni hili, je! Mungu anaruhusu talaka?  Ni mada yenye mvutano mkubwa.Makanisa mengi wanachukulia talaka kama dhambi isiyoweza kusamehewa wakifundisha watu kwamba mkiachana kwa talaka, mtu hawezi kuoa wala kuolewa tena. Lakini je!  Neno la Mungu linasemaje?

Kwangu mimi si swala la kimantiki tu. Nilikuwa nimeshabadilika kuwa Mkristo pale mke wangu wa kwanza aliponiacha akaenda kwa mwanamume mwingine. Baada ya miaka mitatu, nilikutana na mwanamke mrembo aliye sasa mke wangu aitwaye Jacqui. Wakati ule, kama ilivyo hata leo, kilichokuwa muhimu kwangu kilikuwa kumheshimu Mungu kuliko vyote, hata kuliko tamanio langu la kumuoa Jacqui. 

Kwahiyo, jiulize, kwa mfano wangu ule, je! Mimi kuoa tena ilikuwa sambamba na Biblia … au la? 

1 Wakorintho 7:15  Lakini yule asiyeamini akiondoka, na aondoke.  Hapo huyo ndugu mume au nduge mke hafungiki.  Lakini Mungu ametuita katika amani. 

Imeandikwa wazi kwamba kwa mfano huo, aliyeachwa “hafungiki”, ina maana kwamba yu huru kuoa au kuolewa tena.  Lakini yule aliyefanya uasherati huko mwanzoni, hata kama anaoa au anaolewa tena, bado ataendelea kuwa mwasherati – tanzia kubwa mno. 

Lakini nisikilize.  Mungu ni Mungu wa rehema na neema. Talaka na uasherati si dhambi ambazo haziwezi kusamehewa.  Zinaweza kabisa. 

Yesu alikufa pale msalabani ili mtu yoyote akiweka imani yake ndani yake anaweza kusamehewa kabisa. Alimwaga damu yake ili atuoshe tuwe safi. Kwa hiyo kama wewe mwenyewe au mtu unayempenda mnajikuta katika mazingira hayo yenye vurugu … kumbuka hayo: 

Damu ya Kristo inatusafisha na udhalimu wote.  Weka tegemeo lako  ndani ya Yesu. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.