... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kuachana na Maisha ya Uhalifu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Warumi 8:3,4 Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili; ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.

Listen to the radio broadcast of

Kuachana na Maisha ya Uhalifu


Download audio file

Mtu akichunguza vizuri jinsi serekali zetu zinavyopanga sera na kuzipitisha, karibu mara zote ni kukabiliana na matukio tu.  Mtu anafanya kitu ambacho hawapendi, mara moja wanapitisha amri mpya kwa kumzuia.  Swali ni Je!  Hii ni inaleta matengenezo kweli?

Licha ya amri zote zilizoandikwa kwenye vitabu vya sheria, licha ya amri zote zinazopitishwa kila mwaka kwa kukabiliana na uovu unaotendeka … bado uhalifu unazidi kuenea leo.

Leo, kuna watumwa wengi kuliko mara zote katika historia ya dunia yetu.  Pia vurugu nyumbani haijawahi kuwa kali kama ilivyo leo.  Watoto wanazidi kudhulumiwa na kuonewa.  Utapeli wa kupora watu pesa zao unakuwa wa hali ya juu kwa kutumia teknolojia na mbinu mpya.  Sasa, kipi kinachoendela hapo?

Warumi 8:3,4  Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili; ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.

Hata ukizidisha amri, huwezi kudhibiti uovu, kwa sababu wahalifu kamwe hawajatii sheria.  Shida iko hapa.  jibu litatoka wapi?

Mungu alimtuma Yesu kuwa sadaka kwa ajili ya dhambi zetu.  Alitoa uhai wake kuziharibu dhambi zetu, akatusamehe na kutupa msimamo ulio sahihi mbele zake ili tuweze kuishi katika uhuru.

Sheria kama sheria haiwezi kukutendea hayo.  Ni Yesu tu.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy