Kubarikiwa Ukiteswa
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Wafilipi 1:29,30 Maana mmepewa kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, ila na kuteswa kwa ajili yake; mkiwa na mashindano yale yale mliyoyaona kwangu, na kusikia kwamba ninayo hata sasa.
Tunapopitia vipindi vya mateso hatuwezi kufikiri kwamba mateso yanaweza kuwa baraka kwetu, ni nani angetumia maneno hayo mawili kwenye sentnsi moja, “mateso” na “baraka”.
Tunapotazamia mambo yajayo, daima tunaota yaliyo mema, yaani mibaraka. Hakuna anayeweza kuomba apate mateso, na kwa kuwa hakuna anayependa kuteswa, ni rahisi kutokuelewa vizuri swala nzima la baraka na mateso.
Mtume Paulo alikuwa mtu aliyezoea zaidi ya wengine kupokea baraka na mateso pia. Hatimaye alikuwa na mtazamo huu:
Wafilipi 1:29,30 Maana mmepewa kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, ila na kuteswa kwa ajili yake; mkiwa na mashindano yale yale mliyoyaona kwangu, na kusikia kwamba ninayo hata sasa.
Kwanini Mungu amekubariki? Amekubarikiaje? Je! Ni kwa niaba ya kumtumikia Kristo? Baraka zake hazitakiwi zikwamie kwako, bali umezipokea ili ziweze kutoka kwako kwenda kwa wengine kwa utukufu wa Mungu. Hii ni pointi ya kwanza.
Pili, ni kwamba pamoja na mibaraka yake, umepewa fursa na heshima kwa kuteswa kwa ajili ya Kristo wakati baraka zile zinakwenda kwa wengine. Kwahiyo, ukipitia kipindi kigumu tena, kumbuka hili: Mtu akiteswa kwa ajili ya Kristo akiwa na moyo safi na kuendelea kuruhusu baraka ziende kwa wengine wakati bado anaumia … yote mawili yatamletea utukufu Kristo.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.