... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Dalili za Ugonjwa wa Mji wa Stockholm

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

2 Petro 2:19 (Waalimu wa uongo) watawaahidia uhuru, nao wenyewe ni watumwa wa uharibifu, maana mtu akishindwa na mtu huwa mtumwa wa mtu yule.

Listen to the radio broadcast of

Dalili za Ugonjwa wa Mji wa Stockholm


Download audio file

Ni ajabu namna ambavyo mwanadamu anaweza kuzoea usumbufu na matatizo – hadi kufikia hatua  ya kutokujali  kiasi kwamba asitake hata kuachana na hali hiyo ngumu.

Mwaka 1973, Jan-Erik Olsson aliteka nyara wafanyakazi wanne wa benki kubwa ya Sweden kwenye jiji la Stockholm baada ya kushindwa kuiba pesa.  Yeye na mwenzake waliendelea kuwateka hao wafanyakazi wa benki kwa siku sita kwenye ghala lililokuwepo chini ya benki. Walipoachliwa hakuna hata mmoja aliyekubali kuwa shahidi wa kuhukumu kwa watekaji hao.  Hata hivyo walianza kukusanya michango ya kuwatetea! 

Hapo ndipo watu walipoanza kusema, hali hiyo ni “Dalili za Ugonjwa wa Stockholm” yaani watekaji wanaanza kutetea watekaji wao. 

Ni kama haieleweki kabisa, sindiyo?  Lakini mimi ninajiuliza kama hali hiyo ni ainisho sahihi kabisa kuelezea jinsi tunapenda kuambatana na dhambi ambayo imetuteka nyara pamoja na kuambatana na watu waliotupotosha. 

2 Petro 2:19  (Waalimu wa uongo) watawaahidia uhuru, nao wenyewe ni watumwa wa uharibifu, maana mtu akishindwa na mtu huwa mtumwa wa mtu yule. 

Haieleweki kabisa kuona namna tunavyoweza kuambatana na dhambi inayotuharibia maisha, dhambi inayoweza kusababisha tusipate kuishi milele mbele za Mungu.  Lakini, kila mmoja wetu anaweza kufahamu vizuri dhambi kadhaa zinazomtawala. 

Lakini acha nikupe habari njema.  Yesu alikuja ili akuweke huru – huru kabisa, utoke chini ya nguvu za dhambi zinazotawala maisha yako.  Usikubali kushikwa na ugonjwa wa Stockholm wa kuambatana na kitu kinachokuharibia maisha. mgeukie Yesu Yeye akikuweka huru, utakuwa huru kabisa. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.