... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kudanganywa kwa Urahisi

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Waefeso 6:17 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu.

Listen to the radio broadcast of

Kudanganywa kwa Urahisi


Download audio file

Acha nikushtue kidogo kwa kukuuliza, je!  Unaonaje nikisema kwamba Mkristo awaye yote asipotambua kwamba anaishi katika eneo la vita ya kiroho?

Kwa hiyo, nikuulize tena, unaonaje?  Ukristo wote umejumlishwa kwa kanuni mbili tu – umpende Mungu na nafsi yako yote na umpende jirani yako kama unavyojipenda. 

Kanuni hizi zinasisika kuwa wazi … lakini katika ulimwengu hisia hua zinakandamiza maadili, nakufanya kanuni hizi kuwa vigumu.  Kumpenda Mungu, kuwapenda wanadamu … kwa kweli ni kazi gumu.  Itamgharimu yule anayejaribu kuzifuata kanuni hizo.  

Nilimsikiliza mtu mmoja akisema kwamba wahudhuriaji wa makanisa wanadanganywa kwa urahisi, kwa sababu hawajifunzi Neno la Mungu. Hali hii inazidi kuonekana siku hizi. 

Msamaha, wema, kujitoa, heshima, ukarimu … maadili hayo yanatoweka siku hizi, si katika jamii kwa ujumla tu, lakini pia ndani ya kanisa, jambo ambalo linahuzunisha sana. Mmmmmh.  Tunawezaje kurejea kwa maana halisi ya kuwa mfuasi wa Yesu … ? 

Waefeso 6:17  Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu. 

Ujue kwamba ndani ya Kristo umesamehewa, umeokolewa, umeitwa uishi maisha mapya, ukiwa umebarikiwa kuwa na uzima wa milele mbele zake.  Halafu ujue Neno la Mungu wewe mwenyewe ili usidanganywe, ili uweze kuishi maisha ya kumpenda yeye na jirani yako pia. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy