... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kudhamiria Kutenda Dhambi

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Warumi 6:1,2 Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?

Kila mmoja wetu anao udhaifu fulani, yaani upungufu ule, dhambi ile moja inayorudi kutusumbua na kukwamisha safari yetu ya imani.  Nadhani unaijua ile dhambi inayokusumbua daima.

Kwa kweli udhaifu wangu ninaufahamu vema.  Na mtindo unaotendeka hapo mtu akijaribiwa na dhambi ile ni kuikataa kwanza, mfano jaribu la kupiga umbeya, au jaribu la kutokuwa mwaminifu kwa pesa  au jaribu lo lote lile.  Lakini jaribu hua linazidi kuwa na nguvu.

Halafu mtu anakumbuka kwamba, hata iweje, Mungu atamsamehe kwa sababu anamwamini Yesu – Kumbe!  Nilikuwa nimeshasahau hilo! – hapo ndipo mtu anajipatia kibali akidhamiria kukubali kushawishika akijua kwamba baadaye atatubu tu.  Je!  Umeshafikiria hayo?

Jamani!  Muda umewadia kuwa makini.

Warumi 6:1,2  Tuseme nini basi?  Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi?  Hasha!  Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?

Hili ni swali muhimu, kama hukuelewa.  Tutaishije? Ni neno analotwambia Mungu kupitia Mtume Paulo.  Utawezaje wewe kufanya hivyo baada ya mimi kukutendea yale yote nilyoyakufanyia wakati nilimtoa Yesu kufa pale msalabani afe kwa ajili yako?  Ungethubutuje?

Neema ya Mungu si kibali cha kuendelea kutenda dhambi.  Siyo leseni inayoturuhusu kushindwa na ile dhambi moja tena na tena.  Kwa hiyo, wakati utadhamiria kujipa kibali cha kutenda dhambi, Roho Mtakatifu akukumbushe jibu la Mungu mwenyewe:

Unawezaje kuthubutu?

Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy